Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MORINHO ATAAMUA MATOKEO YA MECHI YA LEO

Jose Morinho kocha wa Man U
Na; Imani Kelvin Mbaga
,
Usiku wa leo katika ligi kuu ya Uingereza "EPL" kutakuwa na mpambano mkali kati ya timu ya Manchester United au "mashetani wekundu" kama wanavyojiita ambao watakaribishwa na Liverpool katika jiji la Liverpool uwanja wa Anfield.
   Hii ni mechi ya kihistoria na ni mechi inayobeba hisia kubwa kwa wapenzi na mashabiki wa soka hususani walio nchini Uingereza kama siyo duniani kwa ujumla.
   Hii ni mechi ya watani wa jadi licha ya kwamba kila timu ina mtani wake ambaye anatengeneza naye mchezo uitwao "derby" ambapo Manchester United watani wao ni Manchester City huku Liverpool watani wao ni Everton.
  Lakini mechi kati ya Liverpool na Manchester United inabeba hisia kubwa kutokana na historia ya majiji hayo mawili nchini humo. Kabla jiji la Manchester halijawa na miundo mbinu mizuri ya kiuchumi wakazi wake haswa wafanyabiashara walitegemea bandari na miundo mbinu mingine kutoka ktk jiji la Liverpool. Baada ya Manchester kujenga bandari na kuimarisha jiji lao walianza kujitegemea na hilo ndilo lililoanzisha uhasama kati yao kiasi cha kuhamishia uhasama huo kwenye mchezo wa mpira na kusababisha timu zao kuwa na upinzani wa jadi.
    Mchezo wa leo unakuja huku kukiwa na maneno mengi kuhusiana na mwamuzi wa mchezo huo ambao unazikutanisha timu hizo zikiwa kwenye viwango tofauti toka ligi imeanza. Liverpool wanaolilia taji la 19 la ligi hiyo baada ya miongo zaidi ya miwili toka walipofanya hivyo.
   Manchester United nao wanataka kurejea katika zama zao baada ya kutofanya vizuri kwa zaidi ya misimu zaidi ya minne toka alipoondoka kocha maarufu wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson.
Jurgen Klopp kocha wa timu ya Liverpool
                                                   Mchezo wa leo tunategemea kuona timu zote mbili                                   zikitafuta ushindi ili kujiweka vizuri katika msima wa ligi ili kila mmoja ajiweke katika mazingira bora ya kuklidhi kiu ya mashabiki wa timu zao.
   Endapo Jose Morinho ataamua kumtumia Paul Pogba katika eneo la kiungo cha kukaba samba na ama Maruan Fellain au Carrick au Herera basi Manchester United watakuwa na tatizo kubwa sana kwenye kuzuia kasi wachezaji wa Liverpool wenye kasi kubwa kama Fellipe Cotinho.Sadio Mane pamoja na Roberto Firmino ambao wote wana kasi kubwa hasa wanapovuka mstari wa kati ya uwanja kuelekea eneo la tatu la timu pinzani.

Bila shaka Jose Morinho ana njia moja tu ya kufanya nayo ni kukaba kwa nguvu kuhakikisha viungo wa Liverpool hawapigi pasi ndefu au hawapitishi mipira kwenye nafasi wakati wa kusonga mbele, njia nyingine ni kutoruhusu wachezaji wa Liverpool wa pembeni hawapati nafasi ya kukimbia na mpira. zaidi sana Itabidi awaambie wachezaji wake wachukue tahadhari kuwadhibiti wachezaji wa Liverpool kutofanya maamuzi katika eneo lao la tatu.
   Tunatazamia mchezo wa kukata na shoka pale Anfield mcheo ambao naamini matokeo yake yataamuliwa na mbinu za makocha wa pande zote mbili

3 comments:

  1. Kikubwa mimi km mshabiki wa Arsenal naomba timu hizo zitoke sare tu au Man United afe

    ReplyDelete
  2. Haina namna Liverpool chapa hao wazee wa Media na Klopp endeleza ufalme wako kwa Mourinho

    ReplyDelete

Powered by Blogger.