Mwenyekiti wa mtaa wa Mwembeni kata ya Manzese RESTORY KOBELO Awapongeza wananchi wake kwa Kujitokeza Kwa wingi Siku ya Upandaji miti Oktoba Mosi
Na Mainda Marijani, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa mtaa wa mwembeni kata ya Manzese, wilaya ya Ubungo jijini Dr es salaam, RESTORY KOBELO, amewapongeza wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upandaji miti lililofanyika tarehe mosi mwezi oktoba 2016.
Akizungumza na Tanganyika FM mwenyekiti huyo alisema kuwa zoezi hilo litasaidia kuboresha na kutunza mazingira kwa kuwa kila mkazi anatambua thamani ya miti hiyo.
“ nafurahi kwa namna wananchi wangu walivyojitokeza na kuonesha ushirikiano katika siku hii muhimu na kukamilisha suala hili naamini tutaitunza miti hii kwa pamoja ili iweze kukua,” alisema Kobelo.
Aidha mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kuwa anatarajia kuandaa sheria na kanuni ambazo kila mtu atawajibika kuzitekeleza.
“ Ninaandaa sheria na kanuni za utunzaji miti endapo atabainika mtu yeyote atakaye kiuka sheria hizo basi hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema mwenyekiti.
Kwa upande wake mkazi wa eneo hilo ZAMDA HUSSEN alisema kuwa uonguzi ulisimama imara kaitika kukamilisha zoezi hilo na mambo yote kukaa sawa siku hiyo pasipo vurugu ya aina yoyote.
“endapo tukidumisha ushirikiano kati yetu na viongozi itatusaidia kupiga hatua mbele katika kutafuta maendeleo ya kata yetu na siyo utendaji wa upande mmoja.” Alisema Hussein.

Post a Comment