Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

POLISI:TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAMASUMBWI THOMAS MASHALI ZINATOLEWA KESHO


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na upelelezi  kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa taarifa ya kifo hicho siku ya  kesho Jumatano.
 
Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alisema taarifa zilizopo kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu, hivyo Jumatano atatoa taarifa hiyo.
 
Kamishina Sirro alisema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya mtaani tu.

No comments

Powered by Blogger.