WAKAZI WA MTAA WA SINZA D WALALAMIKIA KUTOPATA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KWA WAKATI
Na Mainda
Marijani,Dar es Salaam.
WAKAZI wa Mtaa wa Sinza D kata ya Sinza wilaya ya
Ubungo Jijini Dar es Salaam wameulalamikia uongozi wa mtaa huo kutokana na kutotoa kwa wakati taarifa juu ya ufafanuzi wa wa mapato na matumizi ya serikali ya mtaa
huo.
Akizungumza
na Tanganyika Fm mmoja wa wananchi hao bw. Christopher Osmond amesema baadhi ya
wananchi katika eneo hilo wanashindwa kupata taarifa hizo kwa wakati muafaka
kutokana na Utaratibu uliopo sasa ambao si mzuri katika kutoa taarifa za mapato
na matumizi hivyo ameshauri uongozi wa mtaa
kuweeka utaratibu unaeleweeka.
“ Baadhi ya
watu hawajui kusoma hatimaye hukosa kujua kinachoendelea katika maeneo
wanayoishi hivyo tunaomba serikali ya
kata itusaidie kufafanua na kutoa taarifa kwa wakati,” alisema Osmond.
Naye katibu
mtendaji wa ofisi ya kata akizungumza
kwa niaba ya Afisa mtendaji bi. Zawadi Ayubu alisema wao hupata taarifa kutoka
serikali za kata na kuzifikisha manispaa na baada ya hapo taarifa hizo hubandikwa
katika kuta za ofisi yao.
Hata hivyo
ametoa wito kwa wakazi wa mtaa huo kuwa na utaratibu wa kuchangia huduma mbali
mbali katika mtaa huo kwa lengo la kuhakikisha gurumdumu la maendeleo linasonga
mbele.
Aidha ameongeza
kuwa muitikio kwa wananchi ni mzuri na changamoto hazikosekani lakini kwa
kiwango kikubwa wananchi hao wana uelewa wa kutosha juu ya masuala mbali mbali
na kuwataka kushirikiana kikamilifu na uongozi ili kukabiliana na changamoto
hizo.

Post a Comment