Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

WAZIRI WA FEDHA DK MPANGO AMWAKILISHA RAIS MKUTANO WA TANO WA USHIRIKIANO KATI YA NCHI ZA KIAFRIKA NA KOREA KUSINI

Na Joseph Peter Maelezo.

MKUTANO wa Tano wa Ushirikiano kati ya Nchi za Kiafrika na Korea Kusini (Korea-Africa Economic Cooperation (KOAFEC), Umefunguliwa leo Jijini Seoul, Korea Kusini, huku agenda kubwa ikiwa ni kuzungumzia namna nchi za Kiafrika zinavyoweza kutumia kilimo katika muktadha wa maendeleo ya viwanda ili ziweze kujikwamua haraka kiuchumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, anawakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) katika mkutano huo unahusisha nchi 54 za kiafrika na nchi ya Korea Kusini.

Dkt. Mpango ameuelezea mkutano huo ulioandaliwa na Serikali ya Korea Kusini kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya EXIM ya nchini humo, kwamba utaleta mapinduzi makubwa katika nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kilimo, rasilimali watu na teknolojia ya habari na Mawasiliano-TEHAMA.

Amesema kuwa nchi ya Korea Kusini ilipata uhuru mwaka mmoja na nchi ya Ghana, Mwaka 1954 miaka michache kabla ya Tanzania Bara kupata uhuru wake, lakini imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kuwa moja kati ya nchi za ulimwengu wa kwanza kiuchumi, lakini Ghana na Tanzania bado ni nchi masikini.“Ni jambo zuri kwamba tuimarishe ushirikiano na Korea Kusini ili njia walizotumia kupiga hatua kubwa kimaendeleo, na sisi tuweze kujifunza kwa haraka” alifafanua Dkt. Mpango.

No comments

Powered by Blogger.