Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

HATUA ZICHUKULIWE KUKABILIANA NA TSUNAMI

Na Joseph Peter.
Tarehe 5 Novemba ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya kimataifa ya mara ya kwanza kuhamasisha dunia kuhusu athari za Tsunami,

Maadhimisho haya hufanyika kila tarehe tajwa mwezi novemba kila mwaka lengo likiwa ni kukumbushana juu ya Tsunami. 

Tsunami ni mfululizo wa mawimbi yenye dhoruba ambayo hutokea chini ya bahari ghafla na huwa na uharibifu pamoja na madhara makubwa zaidi. 

tsunami iliyoacha kumbukumbu  milele ni ile  iliyotokea mwaka 2004 katika Bahari ya Hindi, na kuua watu 230,000.

Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa upunguzaji wa hatari ya majanga Robert Glasser, ameonya dhidi ya kulegeza hatua, wakati huu ambapo kuna tishio la kimataifa la tsunami.

Akizungumza huko New Delhi, India katika mkutano wa ukanda wa Asia wa mawaziri wanaoshughulikia upunguzaji wa hatari ya majanga Bwana Glasser amenukuu ripoti mbili za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa matukio ya tsunami yanaweza kutokea katika maeneo mengi duniani.

Hata hivyo amesema Ulaya na Amerika ziko hatarini sambamba na nchi zinazozunguka bahari ya India na Pasifiki.

Naye mwandishi mkuu wa moja ya tafiti hizo, Profesa Fumihiko Imamura amesema ni muhimu kuhamasisha dunia kuhusu athari za Tsunami na watu lazima waelewe cha kufanya na wapi pa kwenda mara moja kengele ya tahadhari inapotolewa.

No comments

Powered by Blogger.