MAREKANI IMEFUNGA KWA MUDA UBALOZI WAKE NCHINI KENYA
Marekani imeamua kufunga kwa muda Ijumaa hii ubalozi wake nchini Kenya kufuatia kisa cha kijana mmoja kupigwa risasi Alhamisi hii Oktoba 27 alasiri mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, baada ya kujaribu kumchoma kisu polisi wa Kenya ambaye alikua akitoa ulinzi kwenye eneo kunakopatikana ubalozi huo.
Uchunguzi umeanzishwa, lakini hakuna dalili yoyote inayoonyesha kama ilikua shambulizi la kigaidi.
Polisi aliyekuwa amelengwa ni kutoka kikosi chacha kijeshi cha polisi wa Kenya (GSU), wanaohusika na kutoa ulinzi katika eneo lililo karibu na ubalozi wa Marekani.
"Ni mpita njia ambaye alikuwa akitembea katika mtaa wa Umoja wa Mataifa, alimshambulia kwa kisu mmoja wa askari polisi, alimchoma kisu kichwani, amesema Vitalis Otieno, mkuu wa polisi wa eneo la Gigiri. Polisi huyo alijihami kwa kumpiga risasi mtu huyo na kufaulu kumuua. "
Afisa huyo aliyejeruhiwa alipelekwa mara moja hospitalini ambapo anaendelea vizuri kwa mujibu wa viongozi.
Mashahidi katika eneo la tukio wamesema kwamba mshambuliaji anayeonekana kutoka kabila la Somalia, alimshambulia polisi kwa kisu. Mfanyakazi wa mgahawa uliyo karibu na eneo la tukio ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa aliona polisi akimpiga risasi mtu mmoja ambaye alikua na kisu mkononi baada ya kudondoka.
Kijana huyo ana umri wa miaka 24 na ni kutoka kaunti ya Wajir inayopakana na Somalia, polisi imesema, huku ikikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu chanzo cha tukio hiloWakati huo huo
Taarifa hii ni kwa msaada wa: RFI
Post a Comment