DSTV YAJA NA ZAWADI KWA WATEJA WAKE, JOTI KUIPAISHA TANZANIA
Lucas Mhavile "JOTI" balozi wa DStv Bomba |
Na; Imani Kelvin Mbaga
Kampuni ya
MULTCHOICE Tanzania imeamua kutoa zawadi ya sikukuu kwa wateja wake kwa
kupunguza bei katika kifurushi cha DStv bomba ikiwa ni pamoja na kuongeza
chaneli nyingi zaidi kwenye kifurushi hicho.
Hayo
yamebainishwa leo na meneja mwendeshaji wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo,
akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena wakati wa hafla ya
kumtambulisha balozi mpya wa kampuni hiyo msanii wa vichekesho hapa nchini,
Lucas Mhavile (Joti).
DStv ambao
wapo katika mkakati wa kuboresha huduma zao hapa nchini, wametangaza punguzo la
kifurushi cha DStv bomba ambacho hapo kabla kilikuwa kinalipiwa shilingi
23,500/- za kitanzania na sasa kitalipiwa shilingi 19,975 na bei hiyo inaanza
leo tarehe 15 Novemba.
Ronald Shelukindo meneja mwendeshaji wa MULTICHOICE Tanzania |
Pamoja na
punguzo hilo MULTICHOICE pia walitangaza kuongezwa kwa chaneli mpya katika kifurushi
hicho kama vile B4U Movies, SuperSport 4, Eva Plus, Supersport 12, na FoxLife.
Shelukindo
pia alitanabaisha kuwa wateja wa kampuni hiyo wataendelea kupata burudani ya matangazo
ya mpira ya moja kwa moja “live” ya ligi ya England “EPL” ikiwa ni pamoja na
michuano ya ligi ya Hispania “La Liga” kwa mara ya kwanza bila ya kusahau kombe
la mataifa ya Afrika “AFCON” yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon kuanzia January 2017.
Katika hatua
nyingine kampuni hiyo imemtambulisha rasmi msanii wa vichekesho nchini Tanzania,
Lucas Mhavile maarufu kama JOTI kwa jina la kisanii kuwa balozi wao katika kutambulisha
na kutangaza kifurushi hicho cha DStv Bomba na atasaidia kutangaza kifurushi
hicho.
Akiishukuru
kampuni hiyo, JOTI alisema kuwa ni fahari kwake kufanya kazi na DStv hasa
katika bidhaa inayowajali watu wa kawaida wenye kipato cha kawaida kama yeye na
kwamba atafanya kazi hiyo kwa nguvu.
“nilifurahi
sana nilipoambiwa kuwa natakiwa kuwa balozi wa DStv, na mimi ni msanii na hali
yangu ni sawa na watu nitakaowatumikia katika jukumu langu hili, nashukuru
kwamba na DStv wameamua kuwakumbuka watu wa kawida” Alisema JOTI.
Post a Comment