INIESTA AREJEA KUNOGESHA EL-CLASSICO
![]() |
Andres Iniesta nahodha wa Barcelona |
Na: Imani Kelvin Mbaga
Kiungo mahiri na nahodha ya klabu ya Barcelona, Andres Iniesta ambaye amekuwa nje ya dimba kwa muda mrefu, sasa anatarajiwa kuwa vizuri kuwavaa Real Madrid katika mechi kubwa maarufu El-classico.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Barcelona, Iniesta anaendelea vizuri na mazoezi na kwamba atakuwemo katika kikosi kitakachokwaana na watani wao wa jadi Real Madrid wanaoongoza ligi ya Hispania kwa sasa La liga.
Iniesta hajaonekana dimbani kwa muda mrefu na pengo lake limekuwa likioneka kutokana na kukosekana kwa ubunifu katika eneo la kiungo.
Taarifa za kurejea kwake zimepokelewa kwa furaha kubwa na wapenzi wa klabu hiyo ulimwenguni kote, ambao wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na namna wapinzani wao wanavyofanya vizuri.
Post a Comment