LEO USIKU WA UEFA EUROPA LIGI: KARATA YA MWISHO MAN UNITED KUIVAA FEYENOORD OLD TRAFFORD, WAKITELEZA NJE!
Manchester United Leo wanatinga Uwanjani kwao Old Trafford kucheza Mechi yao ya 5 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI wakisaka ushindi ili kujiweka hai kwenye 2 Bora ambazo zitaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Hii ni moja ya Mechi zote za 5 za Makundi zinazochezwa Leo na baada ya hii kila Timu itabakiza Mechi 1 tu itakayochezwa Desemba 8.
Kwenye Kundi A, Man United wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Fenerbahce wenye Pointi 7 kama vile Feyenoord.
Man United, ambao wameshinda Mechi zao zote 2 za Kundi A walizocheza Old Trafford na Fenerbahçe na Zorya Luhansk, Leo wanacheza na Feyenoord ambayo, bila kutegemewa, iliifunga Man United 1-0 huko Rotterdam Mwezi Septemba kwenye Mechi ambayo Man United na walistahili kushinda.
Meneja wa Feyenoord, Giovanni van Bronckhorst, Mchezaji wa zamani wa Arsenal, anaihofia Man United akitegemea kusulubiwa na hata fomu ya Timu yake sio nzuri kama mwanzoni mwa Msimu waliposhinda Mechi zao 11 za kwanza kati ya 12, moja ikiwa dhidi ya Man United.
Lakini hivi karibuni wameshinda Mechi 1 tu kati ya 5 ingawa Wikiendi iliyopita waliipiga 3-0 PEC Zwolle kwenye Ligi ya kwao Holland.
Wakati Feyenoord itawakosa Terence Kongolo na Eric Botteghin kutokana na Majeruhi na kufungiwa, Man United Majeruhi wao ni Eric Bailly na Chris Smalling wakati ipo hatihati kwa Marouane Fellaini kucheza kutokana na Musuli za Mguu kumsumbua.
Meneja wa Man United, Jose Mourinho, anatarajiwa kubadili Kikosi toka kile kilichotoka 1-1 na Arsenal na mmoja wa Wachezaji ambao watacheza hii Leo ni Henrikh Mkhitaryan ambae amekuwa hachezeshwi na pia Zlatan Ibrahimovic alieikosa Mechi na Arsenal kwa kuwa Kifungoni.
KUNDI A – Mahesabu ya Kufuzu:
-Ikiwa Fenerbahçe watashinda na Man United kufungwa, Fenerbahçe watasonga
-Hii Leo, Feyenoord na Fenerbahçe zikishinda, United na Zorya zote nje.
Kwenye Mechi nyingine ya Kundi A, Fenerbahçe wako kwao Uturuki kuivaa Zorya Luhansk ya Ukraine.
MSIMAMO - KUNDI A:
EUROPA-A-NOV24
VIKOSI:
Man United: De Gea – Valencia, Jones, Bailey, Rojo – Pogba, Herera – Mata, Rooney, Mkhitaryan – Ibrahimovic
Feyenoord: Jones – Van der Heijden, Nelom, Botteghin, Karsdorp – El Ahmadi, Kujit, Vilhena – Elia, Jorgensen, Toornstra
REFA: Manuel Grafe (Germany)
UEFA EUROPA LEAGUE
Ratiba:
Alhamisi Novemba 24
***Saa za Bongo
KUNDI A
1900 Fenerbahçe v Zorya Luhansk
2305 Manchester United v Feyenoord
KUNDI B
1900 FC Astana v Apoel Nicosia
2305 Olympiakos v BSC Young Boys
KUNDI C
1900 FK Qabala v RSC Anderlecht
2305 Saint-Étienne v Mainz 05
KUNDI D
1900 Zenit St Petersburg v Maccabi Tel-Aviv
2305 Dundalk v AZ Alkmaar
KUNDI E
2305 Austria Vienna v Astra Giurgiu
2305 Roma v Viktoria Plzen
KUNDI F
2305 Athletic Bilbao v Sassuolo
2305 KRC Genk v Rapid Vienna
KUNDI G
2100 Ajax v Panathinaikos
2100 Celta Vigo v Standard Liege
KUNDI H
2100 KAA Gent v Sporting Braga
2100 Shaktar Donetsk v Konyaspor
KUNDI I
2100 FC Schalke 04 v Nice
2100 FK Krasnodar v FC Red Bull Salzburg
KUNDI J
2100 Fiorentina v PAOK Salonika
2100 Slovan Liberec v FK Qarabag
KUNDI K
2100 Hapoel Be'er Sheva v Inter Milan
2100 Sparta Prague v Southampton
KUNDI L
2100 FC Zurich v Villarreal
2100 Steaua Bucharest v Osmanlispor
TAREHE MUHIMU
Droo
26/08/16: Makundi
12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32
24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16
17/03/17: Robo Fainali
Makundi
15/09/16: Mechidei 1
29/09/16: Mechidei 2
20/10/16: Mechidei 3
03/11/16: Mechidei 4
24/11/16: Mechidei 5
08/12/16: Mechidei 6
16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza
23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
Post a Comment