Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

TANZIA: MZEE JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA, RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI



 Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika Serikali ya awamu ya tatu  Mhe. Joseph Mungai (pichani), amefariki dunia jana majira ya saa 11 jioni.

Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alisema kuwa marehemu Mungai amefikishwa katika hospitali hiyo akiwa tayari amekwisha fariki na kwamba kwa upande wao hawajatoa matibabu yoyote zaidi ya huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)

"Ni kweli tumempokea Mungai, lakini alikuwa tayari amekwisha fariki, tunachosaidia sisi ni mochwari tu, kwahiyo kusema kuwa amefia Muhimbili siyo sahihi" Amesema Eligaesha.

Kuhusu chanzo cha kifo chake, Eligaesha amesema hadi sasa bado hakijafahamika, hadi uchunguzi utakapofanyika kwa kuwa hakufia katika hospitali hiyo. "Hatuwezi kusema nini chanzo hilo ni jukumu la familia, na pia kwa kuwa hajafia hapa hatuwezi kujua hadi postmoterm ifanyike, kwa sasa amehifadhiwa hapa" Alimalizia Eligaisha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Chumba cha maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili. Taarifa kamili za msiba huo zitakujia kadri zitakavyokuwa zikitufikia hivyo endelea kufuatilia.

Tanganyikaradio.blogspot inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote katika msiba huu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.  Mungu ilaze roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina



No comments

Powered by Blogger.