Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

EPL MWISHONI MWA JUMA NA MAAJABU YAKE

Penalti iliyosababishwa na Maruan Ferllain
Na: Imani Kelvin Mbaga

Ligi kuu ya kandanda nchini England iliendelea tena mwishoni mwa juma huku kukiwa na matukio mengi ya kusisimua na kustaajabisha sana na kuendelea kuifanya ligi hiyo kuzungumzwa zaidi duniani.

Macho na masikio yalikuwa katika uwanja wa Etihad ambapo wenyeji Manchester City waliwakaribisha vinara wa ligi hiyo Chelsea ambayo ilikuwa inaingia uwanjani huku ikiwa na mwenendo mzuri wa kucheza mechi saba bila ya kupoteza mchezo.

Kipindi cha kwanza kilikuwa cha Manchester City na kipindi cha pili kilikuwa cha Chelsea. Manchester City walikuwa na uwezo wa kumaliza mchezo huo katika kipindi hicho kwakuwa wangeweza kufunga magoli zaidi ya matatu, kitendo ambacho kingewapa wakati mgumu Chelsea.

Kipindi cha pili Chelsea walibadilika na kutumia mashambulizi ya kushtukiza kupata magoli matatu yaliyowapa pointi tatu muhimu zinawafanya kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Moja kati ya madhaifu waliyokuwa nayo City ni kwenye namna ya kukaba kwani Pep Guardiola ameendelea kuuamini mfumo wake wa kumiliki mpira kama njia ya kujilinda, hata hivyo bado mfumo huo umeonekana kuwa na changamoto nyingi ikiwemo uzito wa baadhi ya wachezaji na naina ya ukabaji wanaoufanya.

Mechi nyingine ni ile ya Liverpool ambao walikuwa wanaongoza kwa magoli 3-1 hadi dakika ya 75 lakini hadi mpira unakwisha walijikuta wakiwa wamepoteza mchezo huo kwa magoli 4-3 mbele ya Bournemouth, na kikubwa ni safu ya ulinzi na nafasi ya mlinda mlango ambayo imeonekana kuwagharimu tena.

Uwepo wa Sadio Mane umeonekana kuwa na msaada mkubwa sana kwa klabu hiyo ambayo katioka mchezo wake huo walimkosa kiungo wao mahiri wa Kibrazil Phllipe Corntinho aliye majeruhi.

Jurgen Klopp ana kazi kubwa ya kujiimarisha katika safu ya ulinzi ili kupata watu ambao wana weza kukaba na kulinda ushindi wanaoutengeneza.

Mechi nyingine ni ile kati uya Manchester United ambao hawana msimu mzuri hadi sasa ambao jana walipata sare ya goli 1-1 huku wakiruhusu goli la kusawazisha la Everton kwa uzembe wa mchezaji wa zamani wa timu hioyo Marouan Ferllain aliyeingia na kusababisha penalti iliyozaa goli la kusawazisha.

Yaya Toure bado anahitajiika Man City, JUan Matta bado ni muhimu kwa Man U, wakati ambapo Aguero ni mtui anatakiwa kusaidiwa kisaikolojia, bado Claudiom Bravo hajashawishi watu sababu ya kuondolewa kwa Joe Hart haya ni baadhi ya mafunzo tuliyoyapata kutoka EPL juma hili.
Wachezaji wa Fc Bournemouth wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Liverpool
Kiungo wa Manchester City, Fernandinho akimsukuma mchezaji wa Chelsea Cesc Fabregas na kusababisha kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uluiokwisha kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi uya City

No comments

Powered by Blogger.