Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MULTICHOICE TANZANIA YAWAPA MKONO WA SIKUKUU WATOTO YATIMA






Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akikbidhi msaaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha watoto yatima cha Al-madina kilichopo Tandale

Na: Imani Kelvin Mbaga, Dar es salaam.
Kampuni ya Multchoice Tanzania imefanya ziara ya kijamii na kutoa msaada kwa kituo cha watoto yatima cha Al-madina kilichopo Tandale, katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka na msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya.

Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande, akiambatana na wafanyakazi pamoja na waandishi wa habari, walifika kituoni hapo saa 4:10 asubuhi na kukabidhi zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni tano na kupokelewa na mlezi wa kituo hicho Kuruthum Yusufu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada huo, mkurugenzi huyo wa Multichoice Tanzania, alisema wamekuwa na utaratibu wa kujihusisha na utoaji wa misaada kwenye jamii hasa katika vituo vya watoto yatima kama cha Al-madina ili kuimarisha mahusiano yaliyopo kati yao na jamii.


“Huu ni utaratibu wetu wa kawaida, na kituo hiki ni moja kati ya vituo ambavyo tuna mahusiano mazuri, nah ii siyo mara ya kwanza kwetu kufanya hivi hata mama Kuruthum anafahamu hilo” Alisema mkurugenzi huyo.

“Tulikuja hapa wakati wa sikukuu ya EID na kutoa masaada, lakini pia tumewahi kuwapatia msaada wa cherehani za kushonea nguo kama namna ya kuwasaidia kujitegemea badala ya kutegemea misaada” Aliongeza mkurugenzi.

Naye mlezi wa kituo hicho, Kuruthum Yusufu alitoa shukrani zake kwa Multichoice Tanzania, na kusema kuwa kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao katika nyakati tofauti tofauti, na aliomba wadau wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama Multichoice wanavyofanya.

“tunashukuru sana Mutichoice Tanzania kwa kuwa wahisani wetu wakubwa kila wakati, na hata pale tunapokwama tumekuwa tukiwaomba watusaidie na hawasiti kufanya hivyo” Alisema Kuruthum.

Katika ziara hiyo kampuni ya Multichoice ilitoa msaada wa  vyakula, vinywaji, sabuni na sare zipatazo hamsini za shule kwa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali kutoka katika kituo hicho chenye jumla ya watoto sitini wanaolelewa hapo.
wafanya kazi wa Multichoice wakibeba misaada kabla ya kuikabidhi kwenye kituo cha watoto yatima cha Al-Madina

Baadhi ya misaada iliyotolewa na kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina Tandale kwa Tumbo

Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania, Maharage Chande akikagua kazi za mikono zilizofanywa na watoto yatima wa kituo cha AL-Madina

No comments

Powered by Blogger.