RAIS DKT MAGUFULI AELEKEA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, KWENYE MKUTANO WA 28 WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa
Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia,
kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika
(AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam.PICHA
NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea
Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa
nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea
Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa
nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Comoro
nchini Dk.Ahamada El Badaoui Mohamed katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari
28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea Addis Ababa, Ethiopia,
kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika
(AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya
ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati
akielekea kupanda ndege kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria
Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda
ndege kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa
28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati
akielekea kupanda ndege kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria
Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan atika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea
kupanda ndege kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa
Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 28 Januari, 2017 ameondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako atahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameagwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Paul Makonda.
Pamoja na kuhudhuria Mkutano huo, akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria Mkutano huo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe. Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki tangu aingie madaraka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05 Novemba, 2015
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Januari, 2017
Post a Comment