PROFESA MANYELE:TUNAANZA KUPIMA MADINI KISASA
Serikali kupitia wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali imenunua mtambo mpya na wa kisasa wa uitwao EDXRF ambao utatumika uchunguzi wa kimaabara wa kutambua aina ya madini na kiasi cha madini kwenye sampuli husika.
Amesema hayo leo jijini Dar es salaam mkemia mkuu wa serikali Profesa.Samweli Manyele kuwa mtambo huo utaanza kufanya kazi katika jiji la mbeya ambapo utasaidia pia kurahisisha kutambua madini yalipo ,kulinda afya za watu na mazingira dhidi ya madhara ya kemikali na sheria ya vinasaba vya binadamu sura namba 73 yenye lengo la kudhibiti teknolojia ya vinasaba hapa nchini.
Amebainisha kuwa mtambo huo wa kisasa mbali ya hayo utatumika kuchunguza makosa ya jinai kama dawa za kulevya,sampuli za sumu na nyinginezo ili kutoa majibu yanayowezesha utoaji wa haki katika vyombo vya sheria.
Aidha mkemia mkuu profesa Manyele amesema kuwa mtambo huo umegharimu jumla ya dola 46,266.11 za kimarekani
Post a Comment