Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

ALEX SANCHES AWAPOZA ARSENAL



Katika kile kinachoonekana kama kuwatuliza mashabiki wa klabu ya soka ya Arsenal maarufu kama washika bunduki wa jiji la London kule nchini Uingereza, mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anaechezea klabu hiyo Alexis Allejandro Sanchez ametuma ujumbe kupitia mtandao wa twiter unaosema "coming back home" ikiwa na maana narudi nyumbani ujumbe ulioambatana na picha yake akiwa na wachezaji wenzake wa Arsenal wakishaingilia moja ya mabao waliyofunga katika mechi zilizopita.

Kutumwa kwa ujumbe huo kumechukuliwa kama alama muhimu kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao bado wapo katika sintofaham juu ya mustakabali wa baadhi ya wachezaji nyota wa klabu hiyo ambao hadi sasa hawasaini mikataba mipya na hivyo kuwa kwenye hatihati ya kubaki klabuni hapo.

Wachezaji wengine ambao wapo katika sintofahamu hiyo ni Santi Cazorla, Mesuit Ozil na Hector Bellarin kwa pamoja mikataba yao inaelekea mwishoni huku mazungumzo baina ya bodi ya klabu na wawakilishi wa wachezaji kukwama mara kwa mara na hivyo kutowahakikishia mashabiki wa klabu juu ya hatima ya wachezji wao.

Alex Sanchez aliyehamia klabuni hapo tokea klabu ya Barcelona ya Hispania kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa  paundi milioni 31.7 amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho akiisaidia klabu kunyakua makombe mawili ya FA toka alipowasili.


Sanchez ametuma ujumbe huo akiwa njiani kurejea klabuni hapo akitokea katika majukumu ya kimataifa alikokwenda kuichezea timu yake ya taifa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2018 itakayochezwa huko Urusi. Anatarajia kuwemo katika kikosi cha timu yake pale watakapowakaribisha klabu ya Swansea katika uwanja wa Emirates kaskazini mwa jiji la London Jumamosi ya tar 15 Oct.

Katika michezo ya msimu huu kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amekuwa akimtumia Sanches kama mshambuliaji wa mwisho na kuonekana kufanya vizuri katika nafasi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.