Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

Swali kutoka kwangu…

JPM YANINI KULEA BATA  KWENYE  BANDA LA KUKU?


Na:Nsajigwa Gostance Mwalugaja

Binafsi huwa najiona kama shilingi yenye thamani na bahati kubwa hapa Tanzania,ikumbukwe sifa ya kubwa ya shilingi ni kuwa na pande mbili zenye kunakshi tamaduni na historia ya nchi husika.

Katika makuzi yangu nimebahatika kupata malezi kutoka kwenye familia ya mfugaji, hivyo kunipa fursa kujua aina na tamaduni za mifugo mbalimbali, hususani ngombe, mbuzi, kuku na bata wa aina mbalimbali, kwa faida ya msomaji kuchi ni aina ya kuku wengi wakiasisi uasilia wake na mkoa wa mwanza, tabia nzuri ya kuchi ni kwamba anaumbo kubwa na nyama nyingi wafugaji wengi humfuga kwa madhumuni ya kula nyama na sio biashara kwa kuwa kuchi dume hana tabia ya kupanda mara kwa mara, hii tabia humtofautusha na kuku aina ya kishingo ambae tetea lake hutaga mayai wastani na jogoo aina ya kishingo hupenda sana kupanda matetea wakati wowote.

vivyo hivyo,kuna aina tofauti za bata na tabia tofauti tofauti,pamoja na utofauti uliopo katika aina zao na tabia zao,bata na kuku kila mmoja huwa na tabia moja ambazo huwatofautisha pasipo kuangalia aina ya zao,malezi bata wote hufanana katika malezi ya watoto wao na kuku wote hufanana katika malezi yao .

Bata siku zote hupenda kutanguliza watoto wake katika safari zake katika makuzi yote ya watoto wake lakini kuku yeye hutangulia mbele na kumwaacha vifaranga vyake nyuma,kinadhali binadamu hutafsri malezi ya bata kuwa huwaweka watoto mbele ili kuona adui yeyote wa watoto wake lakini kwa upande wa pili malezi ya kuku hutafsiliwa kuwa hupenda kuhakiki mapito ya watoto wake kabla hawajapita lazima ahakikishe kuwa sehemu hiyo ni salama.

Ufugaji imekuwa ni shughuli rasmi ya kiuchumi na kijamii katika jamii ya kitanzania,binafsi nasema haya kwa kuwa nimebahatika kuwepo katika awamu tano  za uongozi katika taifa langu la Tanzania,nina maana awamu ya kwanza ya mwl. Julius Kambarage Nyerere, awamu ya pili ya mh:alhaji Ally Hassan Mwinyi,awamu ya tatu ya mh: Benjamin wiliam Mkapa, awamu ya nne ya Mh: Jakaya Mrisho Kikwete na awamu ya sasa awamu ya tano ya mh:John joseph pombe magufuli, Katika awamu zote hizi shughuli ya ufugaji imekuwa na mchamgo wa kipekee katika malezi na maendeleo ya kila siku ya watanzania
Katika jamii yetu ya kitanzanzia ,tumekuwa tukiendesha maisha yetu kwa malezi tofauti tofauti ambayo saa nyingine ni vigumu kutofautisha na makuzi ya vifaranga vya kuku na bata,nikiwa kama mwana jamii nimekuwa nashuhudia mambo mengi tofauti tofauti na imenichukuwa muda kutafakari mwisho wa siku najikuta katikakati ya maswali,kati ya maswali mengi nabaki na swali moja kuu,ya nini kulea bata kwenye banda la kuku?maana mambo yamekwa yakiingiliana katika Nyanja zote za kisiasa,kijamii na kiuchumi pia.



Tarehe 14 october kila mwaka taifa la Tanzania huwa tunahadhimisha kifo cha baba wa taifa la Tanzania mwl.Nyerere,natumia mapumziko haya kumuombea kwa mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi lakini pia natumia mapumziko ya maadhimisho ya miaka 17 tangu kifo cha mwl.Nyerere kutafakari baadhi ya mambo aliyoyaasisi moja kati ya mengi mwenge wa uhuru, ambapo siku ya tarehe 14 october mwenge wa uhuru huzimwa.

Tarehe 12 october 2016 rais wa jamhuri ya muungano alifuta safari za maafisa wa serikali waliokuwa wanatakiwa kuudhulia sherehe za kuzimwa mwenge wa uhuru huko mkoani simiu, rais aliagiza maafisa wote waliochukua fedha za safari kuzirudisha na fedha hizo zipelekwe mwenye miradi ya maendeleo.

Hatua ya rais magufuli kufuta safari za maafisa wa serikali kuudhulia sherehe za kuzimwa kwa mwenge wa uhuru, ni hatua ya kizalendo ambayo binafsi naunga mkono kwa asilimia nyingi sana, ni moyo wenye uthubutu pekee utakaothubutu kutoa agizo ambalo kwa namna yoyote agizo hilo linakwenda kuwakwaza wanufaika, kwa namna pekee rais alijaribu kuangalia masirahi yalio ya wengi
Hongera sana rais wane john pombe joseph magufuli, abagunana bhako batamanile echo olelogwa?

Ikumbukwe tangu kuapishwa kwa rais wa awamu ya tano, imekuwa wazi kuwa rais magufuli ni mtu makini sana linapokuja suala la matumizi ya fedha za serikali mara kadhaa amekuwa akitembelea maofisi ya serikali kuhakiki utendaji wa wafanyakazi na matumizi ya mali za umma, hii ni kuhakikisha fedha ya serikali inayopatikana kutokana na kodi ya watanzania inatumika vizuri.

Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa sherehe za muungano zilifutwa mwanzoni wa mwaka huu na fedha zilizotakiwa kufanikisha sherehe hizo ziliamriwa zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo.

hivi ni nani asiekumbuka jinsi mh.rais alivyosimamia kwa nguvu zote suala la wafanyakazi hewa kutoka katika kila idara ya serikali Kwa akili ya kawaida kabisa inajulikana Rais john pombe magufuli hapendi matumizi ya fedha za wananchi ovyo ovyo lakini kwa hatua ya watendaji wa serikali wakiwemo wakuu wa mikoa kupokea fedha za safari za kwenda kuzima mwenge Napata wakati mgumu kidogo kuelewa kama wanaelewa falsa ya kiongozi wao juu ya kubana matumizi ya fedha za umma rais wane, abagunana bhako batamanile echo olelogwa? ilikuwaje wakapokea fedha pasipo kujiuliza faida ya safari zao, wamekosa nini katika utendaji wao, wamekosa kujua falsa ya rais wao, wamekosa mwongozo wa maamuzi yao, wamekosa moyo wa uthubutu wa kushauriana na viongozi wao kabla hawajaamua kufanya jambo?

Naamini hatua hii ya rais kuwaagiza warudishe fedha za serikali haitawapa uoga bali ujasiri wa kufikili na kuchukua maamuzi sahihi baada ya kushirikisha viongozi wao.

Hii ipo wazi siku zote Bata hupenda kutanguliza watoto wake katika safari zake katika makuzi yote ya watoto wake lakini kuku yeye hutangulia mbele na kuwaacha vifaranga vyake nyuma, Napata wakati mgumu kubainisha rais wangu kipenzi una malezi ya aina gani, maana wasaidizi wako nimeshindwa kuwaelewa kwa kushindwa kukuelewa.

kwa asilimia 95 umepunguza safari za nje na ndani za kwako binafsi kwa nia ya kupunguza matumizi ya serikali, umeamua kupita kwanza wewe  ili kuonyesha watumishi wa serikali mapito yalio salama kwa awamu ya tano lakini hii tabia ya wasaidizi wako kuwa mbele wakisubili mwongozo wa kiongozi wao,hii inanichanganya kuku au bata nani anamfumo sahihi wa malezi.

Tatizo ni nini katika hili?tatizo ni kufuga bata kwa malezi na tamaduni za kuku,au tatizo ni nyumba za kufugia hazirandani na tabia za mifungo?

Rais wane, ya nini kusuga mbata mwi banda la ngoko?

Nawasilisha
0713390903
0766610061

No comments

Powered by Blogger.