Asasi Zisizo Za Kiserikali zaadhimisha "Siku ya Afrika ya kutibu Meno bila kutumia dawa yenye Zebaki(mercury)
Na Joseph Peter Dar es Salaam.
Zaidi ya Asasi 40 zisizo za kiserikali ikiwemo AGENDA for Environment and Responsible Development leo hii zinaadhimisha "siku ya Afrika ya kutibu meno bila kutumia dawa yenye zebaki{Mercury} kwa mara ya tatu mfululizo hasa kwa kuziba meno ya watoto.
Serikali za Afrika zimeshauriwa kuacha matumizi ya dawa ya kuziba meno ambayo ina zebaki inayojulikana kwa jina la dental amalgam ili kupunguza matatizo mbali mbali ya kiafya yanayowakumba watoto, Kauli hiyo imetolewa na Afisa program mkuu wa AGENDA Bw. Silvani Mng'anya wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika katika ofisi zao zilizopo Sinza Palestina Mtaa wa Mashujaa jijini Dar es Salaam.
"tunaitaka serikali ya Tanzania na serikali nyingine Afrika Kuchukua uamuzi wa dhati ili kuachana kabisa na matumizi ya dental amalgam kwa ajili ya kuziba meno ya watoto, kidunia Afrika ndiyo inatumia dental amalgam kidogo kuliko mabara mengine hivyo ni kama vile matumizi ya dawa hii yameshapungua barani humu" alisema Bw Silvani.
Baada ya kusainiwa kwa azimio la Abuja "ABUJA Declaration" mwaka 2014 lengo lilikuwa Afrika iwee bara la kwanza kusitisha matumizi ya dental amalgam kwa kuziba meno ambapo Asasi hizo ziliandaa Mpango wa Abidjan ili kusaidia kutekeleza azimio la Abuja na kwa pamoja Asasi hizo zilikubaliana kuwa kila ifikapo tarehe 13 ya mwezi wa kumi kwa kila mwaka iwe ni siku ya kukuza uelewa kwa suala maalumu kuhusiana na kuondoa matumizi ya dawa hiyo katika tiba ya meno.
Zebaki{mercury} ni "madini yenye sumu ambayo huathiri ukuaji wa ubongo wa watoto na mfumo wa fahamu hata kwenye hatua za ujauzito" hii ni kwa sababu Asasi hizi ziliweka siku hii kuzitaka nchi kuondoa matumizi ya dawa hizo katika kuziba meno hasa kwa watoto huku kauli mbiu kwa mwaka huu ikisema "LINDA AFYA YA WATOTO ONDOA DAWA YENYE MADINI YA ZEBAKI{MERCURY} KWA KUZIBA MENO HASA YA WATOTO".
Kwa upande wake Rais wa chama cha madaktari wa meno hapa nchini{TDA} Dr. Lorvina Carneiro amesema kuwa elimu inahitajika kwa wadau na Asasi mbali mbali kuhusu namna ya kupunguza matumizi ya zebaki na kuwa mpaka sasa hivi Tanzania ni asilimia ndogo sana ya watu wanaotumia zebaki katika tiba hasa kwa wale ambao wameathirika zaidi tofauti ikilinganishwa na yale ambayo yameng'olewa kutokana na upatikanaji wa vifaa vya kutolea tiba kuwa ni haba hasa vifaa vya kutobolea meno pamoja na kile cha kuchanganyia zebaki kuwa ni hospitali chache zina vifaa hivyo.
Amesema kuwa kwa sasa wao kama waataalu wanaona bado kuna haja ya kuendelea kutumia zebaki kutokana na kuwa bado haijapatikana njia mbadala ya kutibu meno zaidi ya hiyo inayotumika kwa sasa hivyo ametoa ushauri kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kupiga mswaki angalau mara mbili kwa siku pamoja na kutumia dawa sahihi kwa ajili ya kutibu meno vile vile kuwa na utaratibu wa kupima Afya ya kinywa kwa mwaka mara moja ili kupunguza tatizo hili.
Afisa program mkuu wa AGENDA Bw. Silvani Mng'anya wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika katika ofisi zao zilizopo Sinza B Mtaa wa Kumekucha jijini Dar es Salaam.
Aidha kwa upande wake Afisa afya mkuu kutoka Wizara ya Afya(MOHCDGEC) Anne Sekele amesema kuwa bado kuna tatizo kubwa lililopo kutokana na matumizi ya zebaki na kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii kwa ajili ya utunzaji wa meno hasa ya watoto kwani kuna madhara makubwa ya utumiaji wa madini hayo.
Dental Amalgam ina zebaki kwa kiasi cha asilimia 50 hivyo imeshauriwa hakuna sababu za msingi kuendelea kutumia dawa hii kwa kuwa dawa nyingine ambazo hazina zebaki zipo barani Afrika na duniani kote.
Pia mkataba wa kimataifa wa Minamata uliopitishwa na zaidi ya nchi 140 ikiwemo Tanzania katika mji wa Kumamoto nchini Japan ambao unazzitaka nchi duniani kupunguza matumizi ya dawa hii.
Hadi sasa nchi 128 zimesaini mkataba huu na nchi 32 zimeshauridhia na pia zidhihirishe kimatendo nia ambayo wameionyesha wakati wanasaini mkataba huu.
Tafiti za hivi karibuni zilizofanywa za hivi karibu zilifanywa huko nchini Ivory Coast na Tunisia zinaonesha kuwa tayari takribani asilimia 30 ya madaktari wa meno wanatumia dawa ambazo hazina zebaki pia bado kuna juhudi zinafanyika kila kona na hivyo kuwafanya watu kufahamu athari za zebaki kwa afya na mazingira lakini baadhi ya nchi zinazoendelea na juhudi hizo ni pamoja na Cameroon, Ivory Coast, Guinea,Ghana ,Kenya, Mauritius, Senegal, South Africa,Tnzania na Tunisia.
Ripoti ya shirika la afya duniani (WHO) kuhusu matumizi ya siku zijazo ya dawa za kuziba meno (future use of Materials for dental Restoration) inasema "Dawa zisizokuwa na zebaki zina matokeo sawa na dental amalgam na zina faida kwa afya ya kinywa kwa kuwa zina uharibifu mdogo kwa sehemu ya jino ambayo haijatoboka na hivyo kufanya jino kudumu zaidi.
Mnamo mwaka 2010, nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara zilitumia tani 6 tu za zebaki kwa ajili ya kutibu meno.

Post a Comment