MANJI: WANA YANGA TULIENI, MJE KWA WINGI KWENYE MKUTANO
Yusuph Manji mwenyekiti wa Yanga |
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, Yususph Manji, leo amewataka wanachama wenye mapenzi mema na klabu hiyo kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano ulioitishwa na uongozi wa klabu hiyo siku ya Jumapili tar 23 Octoba mwaka huu katika uwanja wa kaunda yalipo makao makuu ya klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya Twiga na Mafia jijini Dar es salaam leo, Manji amesema maandalizi yote yamekamilika na kila mwanachama wa Yanga mwenye sifa za kuhudhuria mkutano huo anaruhusiwa kuja na kuchangia mawazo ya namna ya kuendeleza klabu hiyo.
"nimesikia maneno mengi sana kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari juu ya mkutano wetu wa Jumapili, lakini nawakaribisha wanachama wote mje kwa wingi kwenye mkutano na kutoa mawazo yenu kwa uhru kabisa" alisema Manji.
Akizungumzia juu ya uhalali wa mkutano huo, Manji amesema kuwa mkutano huo umefuata matakwa ya kikatiba na kwamba lengo ni kuhakikisha kuwa kila mwanachama anpata fursa ya kutoa mchanngo wa maoni ili kuhakikisha klabu inasonga mbele. Pia aliwataka watu wanaotumia vyombo vya habari kulaumu na kuhoji maswala mbalimbali yahusuyo klabu hiyo wanatakiwa kuhudhuria ili kuhoji na kupata majibu juu ya hoja mabalimbali wanazozijadili.
Aidha mwenyekiti huyo alitanabaisha kuwa uongozi wa klabu umeandaa ulinzi wa kutosha ili kuhakikisha kuwa watu wanapata uhuru wa kuchangia mawazo bila ya kubughudhiwa na mtu yeyote. Manji pia alizungumzia suala la watu wanaodaiwa kuwa si wajumbe halali wa bodi ya udhamini wa klabu hiyo na kusema kuwa majina yao yalishapelekwa Rita na hata Baraza la Michezo la Taifa "BMT" na taasisi hizo zipo kimya juu hilo.
"kuna watu wansema kuwa kuna wajumbe wa bodi ya udhamini ambao hawapo hapo kisheria lkn ukweli ni kuwa majina yao tuliyapeleka RITA, BMT na kwingine hawajatujibu tufanye nini?" alihoji Manji.
Akijibu maswali ya waandishi mbalimbali wa habari Manji alisema kuwa suala la uwanja wa m,azoezi wa Geza Ulole ambao ni moja ya mipango ya klabu kwa sasa wanatarajia kuanza kuutekeleza takribani siku tisini baada ya wanachama kuridhia mpango wa ukodishaji wa klabu.
Manji pia alitolea ufafanuzi juu ya umiliki wa eneo hilo na kusema kuwa eneo hilo linamilikiwa na kampuni yake na kwamba hati ya eneo hilo ni mali yake, isipokuwa waliovamia walifanya hivyo wakati kukiwa na marufuku ya serikali ya uendelezaji ili kupisha urekebishaji wa ramani.
Klabu ya Yanga inatajiwa kufanya mkutano mkuu wa dharura siku ya tar 23 Octoba kukiwa na ajenda kadhaa ikiwemo kujadili ikiwa mwenyekiti wao wa sasa Yusuph Manji aendelee na wadhifa wake huo hata baada ya kukodishwa kwa timu hiyo kwa kampuni ijulikanyo kama Yanga yetu Ltd au la.
Licha ya kuwa na wakosoaji wachache juu ya mchakato wa kukodisha klabu hiyo bado wanachama walio wengi wanataka kuona mchakato ukikamilika haraka ili kutoa nafasi kwa uongozi na wakodishwaji wakianza kazi ya kuijenga klabu yao.
Baadhi ya wanachama waliokuwa klabuni hapo wakati na baada ya mkutano huo walisema lengo lao kubwa ni kuona klabu yao inapiga hatua kuelekea kwenye maendeleo na hivyo hawako tayari kukubaliana na watu wachache waliowaita mamluki ambao hawana nia njema na klabu yao.
Wanachama wanaotuhumiwa kuhujumu mchakato wa ukodishaji wa klabu hiyo ni kundi linalojiita kamati maalum ya muafaka ya wazee wa Yanga wakiongozwa na mzee Ibrahimu Akilimali ambaye hata hivyo haijajulikana kama atahudhuria mkuitano wa Jumapili kwa kile kinachodaiwa kutotimiza matakwa ya katiba ambayo inamtaka kila mwana chama kuilipia kadi yake kabla ya mkutano huo.
Post a Comment