Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MKUTANO YANGA WAPIGWA STOP,MANJI AWASHANGAA WAHUJUMU

Yusuph Manji
Na : Imani Kelvin Mbaga

Uongozi wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam umesitisha mkutano mkuu wa dharura uliokuwa ufanyike kesho tar 23 Oktoba katika uwanja wa Kaunda yalipo makao makuu ya klabu hiyo, baada ya kupokea amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kufuatia pingamizi dhidi ya mkutano huo.
   Akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es salaam leo, mwenyekiti wake Yusuph Manji alisema jana saa moja jioni alipokea amri ya Mahakma hiyo ikimtaka kusitisha mkutano huo kufuatia shauri la kuzuia mkutano lililofunguliwa mahakamani hapo na baadhi ya wanachama wakiwepo Frank Chacha, aliyewahi kuwa mwanasheria wa klabu hiyo na Juma Magoma ambaye wakati fulani aliripotiwa kufukuzwa uanachama.
  Akiongea kwa masikitiko mwekiti huyo alionyesha kushangazwa na baadhi ya wanachama aliodai kuwa kuna nguvu inayowasukuma kufanya hivyo kwakuwa baadhi yao wameshindwa hata kulipia kadi zao za uanachama lakini wameweza kulipia gharama za kufungua kesi hiyo mahakamani.
   "jana tulipokea pingamizi dhidi ya mkutano wetu na hivyo hautafanyika kama tulivyopanga licha ya kukamilisha maandalizi yote. Najua kuna nguvu kubwa nyuma ya hawa watu wanaopinga maendeleo ya klabu yetu, baadhi yao wameshindwa hata kulipa ada ya uanachama ya shilingi elfu moja tu kwa mwezi, wamewezaje kulipia gharama ya kufungua kesi?" Alihoji Manji
    Mwenyekiti huyo alisema kuwa wote wenye hoja mbadala wangekuja kutoa hoja zao kwenye mkutano badala ya kukimbilia mahakani kwa kuwa hiyo ni kinyume na katiba ya klabu hiyo kongwe yenye makao yake mitaa ya Twiga na Mafia jijini Da r es salaam.
    "watu wote wanajua ukiipeleka Yanga mahakamani basi unakuwa umejifukuza uanachama wa klabu yetu kwa mujibu wa katiba." Alisisitiza Manji
  "wangekuja kwenye mkutano kwakuwa sisi tuliwahakikishia ulinzi na hata pale ambapo walitaka kutoa hoja kuhusu mimi nilishasema nitatoka nje ya ukumbi wakati wa mjadala unaonihusu mimi" Aliongeza Mwenyekiti huyo
    Katika mkutano huo na waandishi wa habari pia walijitokeza baadhi ya wanacham,a waliotaka kusikia juu ya hatima ya mkutano huo ambao walionyesha kusikitishwa kwao kwa kitendo cha kusitisha mkutano kilichofanywa na wenzao na kudai kuwa watu hao wamekuwa wakitumika kuihujumu klabu, huku wengine wakienda mbali kutaja baadhi ya wafanyabiasha wakubwa (majina tunayo) kuwa ndiyo wahusika wa hujuma hizo
   mmoja wa wanachama hao aliyejulikana kwa jina moja la Jesca alisema wamechoka kuona watu walewale wakitumiwa kuchafua hali ya hewa klabuni hapo.
    "sisi tulishasema mabadiliko ni lazima na hatuko tayari kuchezewa akili na watu wachache wasiotutakia mema" Alisema Jesca
   Uonngozi wa klabu hiyo umewaomba radhi wanachama wote waliosafiri kutoka mikoani kuja kuhudhuria mkutano huo na kuwataka wanachama wote kuwa watulivu huku uongozi wao ukihakikisha unaweka mabo sawa ikiwemo kwenda kujibu hoja mahakamani ili kuhakikisha kuwa haki ya wanachama walio wengi inapatikana

No comments

Powered by Blogger.