MANZESE WALIA NA KERO YA MAJI
Na Mainda Marijani, Dar
Es Salaam
Wakazi wa
eneo la Manzese midizini kata ya Mwembeni, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar Es
Salaam, wamelalamikia suala la ukosefu maji katika eneo hilo, hali iliyopelekea
kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo.
Akizungumza
na Tanganyikaradio.blogspot.com mmoja wa wakazi hao HADIJA RAMADHANI kwa niaba
ya wenzake alisema suala la maji limekuwa changamoto katika makazi yao na
kushindwa kufanya shughuli zao za kujipatia kipato.
“
Tunashindwa kufanya biashara zetu kutokana na kutafuta maji mtaa mwingine na
hata pale maji yanapotoka inatubidi tuache biashara na kwenda kuchota maji hali
inayopelekea kuwa na mauzo mabaya ya biashara zetu,” alisema Ramadhani.
Aidha
ameongeza kuwa serikali ya mtaa ingejaribu kufuatilia suala hilo sehemu husika
ili kufahamu nini tatizo la ukosefu maji katika mtaa huo ingeweza kuwasaidia.
“ serikali
ingekwenda DAWASCO ili kujua nini tatizo na kuweza kulitatua wao kama viongozi
kwa kuwa wana dhamana yetu,” alisema Ramadhani.
Walipotafutwa na Tanganyikaradio blog
viongozi wa mtaa huo na wale wa shirika la maji mkoa wa Dar es salaam DAWASCO
ili kuzungumzia kero hiyo hawakupatikana mara moja na juhudi za kuwapata
zinaendelea ili kutoa ufafanuzi
Post a Comment