MUZAMIRU AIPAISHA SIMBA KILELENI
Na: Imani Kelvin Mbaga
Goli la dakika ya 86 lililofungwa na Muzamiru Yassin kiungo mahiri wa vinara wa ligi kuu ya kandanda ya Vodacom Tanzania bara Simba Sc dhidi ya Mbao fc kutoka Mwanza limezidi kuwaimarisha kileleni baada ya kujikusanyia alama 26 katika michezo kumi iliyocheza hadi sasa.
Muzamiru Yassin aliyesajiliwa msimu huu akitokea timu ya Mtibwa Sugar amekuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya klabu hiyo inayopigania kurejesha heshima yake katika ligi kuu nchini Tanzania.
Simba ilianza mchezo wa leo kwa kasi yake ileile licha ya kupata upinzani kutoka kwa timu ya mbao iliyopanda msimu huu na kuanza ligi vibaya kwa kupoteza michezo mfululizo. Hata hivyo katika mechi ya leo Mbao walionekana kuwa imara kwa vipindi vyote licha ya mara nyingi kuwaacha Simba wakicheza katika eneo lao kiasi cha kuwaruhusu mara nane kuingia ndani ya eneo lao la hatari katika kipindi cha kwanza pekee na kupata kona zaidi ya nne lakini hata hivyo kipindi hicho kilimalizika kwa timu zote kutoshana nguvu bila ya kufungana.
Kipindi cha pili bado mchezo huo ulionekana kutawaliwa zaidi na Simba ambo walionekana kucheza kwa nguvu kuusaka ushindi na alama muhimu tatu kwa siku ya leo. Katika kipindi hicho Simba walifanya mabadiliko yaliyoonekana kuzaa matunda ambapo Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib walitoka na nafasi zao kuchukuliwa na Fredrick Blagnon na Ibrahim Mohamed "Mo" ambao waliongeza kasi ya mchezo na hatimaye zikiwa zimesalia dakika nne za muda wa kawaida kumalizika Muzamiru Yassin alimalizia pasi safi ya Fredrick Blagnon na kuiandikia Simba bao la kuongoza na hadi mwisho wa mchezo huo Simba waliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbao fc.
Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri na wa kusisimua kwa dakika zote na timu ya Mbao ilileta upinzani mkubwa katika mchezo huo ikionyesha kukomaa katika ligi.
Ligi hiyo inatarajiwa kuelendelea mwishoni mwa juma ambapo siku ya jumamosi kutakuwa na michezo minne ambapo African Lyon watacheza na Mbeya City, Azamu na Ruvu Stars, Kagera Sugar na Yanga, Majimaji na Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar na Stand Utd, na Ndanda na Mwadui

Post a Comment