Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MWIGULU AMREJESHA HANS YANGA

Na: Imani Kelvin Mbaga

    Kocha mkuu wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam aliyejiuzulu hivi karibuni, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amebadilisha uamuzi wake huo baada ya kile kinachoelezwa kama  mazungumzo yake na waziri wa mambo ya ndani ya nchi mh Mwigulu Nchemba kuufanikiwa.

  Mazungumzo hayo kati ya waziri huyo anayefahamika kama mwanachama na mpenzi wa Yanga lakini pia mdau wa michezo hususani mpira wa miguu nchini yamefanyika kwa siri kubwa hadi pale matokeo yake yalipokuja kufamika.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYYsM872xVhLG2znaWN04HTNGLINg0lXcMsvEdYzcBfcvvToFX9TDWXIXcvB2mFu30WAnc736iQqhZn2q7_ZJ2qEk7ggjYxf953M3CeAb4B8f550b_-UlRy1CswL9UPkfoaOg7aVJSc6E/h120/babu.jpg
Mh Mwigulu Nchemba akiwa na Hans Plujm
  Hans Van Der Plujm aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake kama kocha mkuu wa mabingwa hao watetezi na kuikabidhi kwa uongozi siku ya tar 22 Oktoba mwaka huu huku kukiwa hakuna ufafanuzi wa kina juu ya sababu za msingi za kujiuzulu kwake ingawa kulihusishwa na mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kati ya klabu hiyo na kocha mkuu wa klabu ya Zesco ya Zambia George Lwandamina.

  Vyombo vya habari viliripoti juu ya ujio wa kocha huyo wa Zesco na kulikuwa na taarifa za kubadilishiwa kwa majukumu kwa Plujm kutoka kuwa kocha mkuu hadi mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo jambo ambalo siyo tu kwamba lilikanushwa na uongozi wa Yanga lakini pia Plujm mwenyewe alionyesha kuto ridhishwa na majukumu hayo mapya.

  Hata hivyo taarifa zilizopatikana asubuhi ya leo ni kuwa waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba aliingilia kati kujiuzulu kwa kocha huyo na kufanikiwa kumshawishi kurejea tena katika nafasi yake hiyo.

Kwa mujibu wa barua iliyopatikana leo jijini Dar es salaam ikiandikwa kwa Hans Plujm na katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit inayotangaua barua ya kujiuzulu kwa kocha huyo na kumshukuru waziri wa mambo ya ndani kwa kuingilia kati suala hilo.

  Hii ni mara ya pili kwa waziri huyo kuingilia kati mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na waajiriwa wake, baada ya kufanya hivyo hapo mwanzo baada ya klabu hiyo kusitisha mkataba wa kiungo maarufu wa klabu hiyo Haruna Niyonzima aliyechelewa kuripoti toka Rwanda alikokwenda kuitumikia timu yake ya taifa.

  Baada ya uongozi wa Yanga kusitisha mkataba wake waziri huyo pia aliripotiwa kuingilia kati mzozo huo hatimaye kumrejesha kikosini mchezaji huyo. Kinachosubiriwa sasa ni kuona kama kocha huyo atarejea kwenye benchi la ufundi katika mchezo wa kesho dhidi ya Mbao au lah.
barua ya Yanga kwenda kwa Hans Van Der Plujm

No comments

Powered by Blogger.