ZANTEL WAJA NA 4G, SASA KUTOA HUDUMA BORA NA YA KASI KWA WATEJA WAKE
Benoit Janan (katikati) Afisa Mtendaji mkuu wa Zantel |
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, imetangaza mabadiliko makubwa ya kiteknolojia ili kuendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya mtandao hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo driving in jijini Dar es salaam kwenye ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo, Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Benoit Janin alisema Zantel imekuwa katika uboreshaji wa huduma zake kwa awamu na kwamba sasa wateja wa kampuni hiyo watafurahia huduma za kasi ya intaneti ya 4G ambayo itapatikana kwa zaidi ya 60% ya maeneo yote ambako huduma za kampuni hiyo zimefika.
"tangu tulipoanza huduma zetu,tumekua tukitoa huduma kwa kiwango bora na cha hali ya juu hususani katika huduma za intaneti kwa wateja wetu hapa Tanzania tena kwa gharama rafiki kwa watumiaji. Ukamilishaji wa huduma hizi za kisasa, haraka na zilizoenea zaidi Tanzania zinatufanya tuwe wa kwanza kwa mara nyingine na kuleta faida halisi kwa wateja wetu" Alisema Janin
Zantel imetangaza kuwa hadi kufikia siku ya Jumapili tar 30 Octoba mwaka huu wateja wa kampuni hiyo wanatakiwa wawe wameziseti simu zao moja kwa moja "automatic" ili waweze kutumia huduma za 4G bila ya usumbufu wowote.
Herbert Louis mkuu wa kitengo cha mauzo wa Zantel |
Akizungumzia juu ya changamoto inayolikabili soko la intanet nchini, Louis alisema kuwa wamefanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha kuwa mtandao wao utakuwa bora na huduma za uhakika kwa wateja wao.
"tumejitahidi kufanya marekebisho makubwa na sasa tuna uhakika kwamba wateja wetu wanaweza kufurahia huduma zetu bila ya wasiwasi na pale wengine wanapokwama basi sisi tumepafanyia kazi ili kuonyesha utofauti wetu na wengine kama ilivyo siku zote" Alifafanua Louis
Zantel wamekuwa katika hatua za uboreshaji wa huduma zao na sasa wametangaza rasmi kuanza kutoa huduma ya 4G kwa wateja wao.
Baadhi ya wateja walioongea na tanganyikaradio.blogspot.com wameonyesha kufurahishwa na hatua ya kampuni hiyo kuboresha huduma zao na kusema kuwa hiyo itawafanya kuendelea kuitumia ili kufaidika na huduma zao kama ilivyokuwa mwanzo ambapo walisema kampuni hiyo iliwafanya kufurahia huduma za mtandao kwa urahisi.
Wateja wa kampuni hiyo wametakiwa kupiga namba 100 ili kupata maelezo sahihi ya namna ya kupata huduma ya 4G kwenye simu zao pale tu wanaposhindwa kufanya hivyo
Post a Comment