NEWZ ALERT:WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA ATOA TAARIFA RASMI ZA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI MKOANI MBEYA
Mnamo Tarehe 26.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwamafunzo.
Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. Septembermwanafunzi hakuonekana shuleni.
Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao.
POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa
mwanafunzi huyo.
MWIGULU Nchemba, W MNN
Heshima yako mh.mwigulu
ReplyDelete