tuseme hapana,yatosha matumizi ya madini risasi ………… NAJIPENDA,NAIPENDA FAMILIA YANGU,NAIPENDA JAMII YANGU
Na: Nsajigwa mwalugaja
| shughuli za uchimbaji wa madini |
Risasi ni aina ya madini chuma yanayopatikana sana katika
tabaka juu la dunia na kusambazwa zaidi duniani na shughuli za kila siku za
mwanadamu.
Madini risasi katika mwili wa mwadamu ni sumu
yanayoshambulia zaidi katika eneo la ubongo wa mwanadamu na kupunguza uwezo wa
kufikiri na kuamua jambo kiufasaha,madhara yake hukuwa mpaka kusababisha kifo.
Madini risasi yamekuwa na madhara kubwa sana kwa watoto
walio chini ya miaka sita na kwa kiasi kikubwa hushambulia ubongo nakudhuru siha
makuzi ya viungo vya mtoto,watoto hupata
madini risasi kwa njia kuu mbili
·
shughuli za upakaji rangi kwenye makazi/kuta
za nyumba zetu na mwilini,kubandika stika mwilini
·
vumbi lililoambatana na madini risasi katika
shughuli za ujenzi
·
mabaki ya mabetri mbali mbali
·
maji yaliopita katika mabomba yaliotengenezwa
na madini ya kopa
·
kuziba meno yalioharibika kwa kutumia madini
risasi
·
shughuli za madini
Dalili za madhara ya madini risasi mwilini
Dalili za madhara ya madini risasi mwilini
·
maumivu ya sio ya kawaida mwilini
·
maumivu ya kichwa mara kwa mara
·
usingizi wa mara kwa mara
·
mwili kutokuwa vizuri
·
kukosa hamu ya kula mara kwa mara
·
shinikizo la damu
·
kupoteza kumbukumbu ovyovyo na kuwa na uelewa
mdogo
·
anemia
·
tatizo la kusikia vizuri
Maadhimisho
ya wiki ya kupinga matumizi ya madini Risasi
kuelekea wiki ya tarehe 23 mpaka 29 ya mwezi October naungana na jamii ya
wanaharakati wa maendeleo ya jamii ktika kupinga matumizi ya madini risasi
ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisambaza sumu mwilini pindi yanapofanikiwa
kuingia katika mwili
Ni vizuri jamii ikafahamu sumu ni nini,katika Kiswahili rahisi
kabisa SUMU ni kitu chochote kinachoweza kuharibu wa kiasi kidogo au kikubwa
seli katika mwili wa mwanadamu au kuweza kudhuru muundo wa seli au kiumbe hai
sumu ina patika na sehemu kuu tatu
·
mboga
·
wanyama kama nyoka,nyuki n.k
·
madini(asenia/zebaki)
nimeanza makala hii kwa kutoa ufahamu dhidi ya madini risasi
kwa kuangali chanzo kikuu katika uenezaji wa madini risasi lakini pia kuanisha
viashiria vya kudhurika na matokeo ya madini risasi ili jamii iweze kutambua
madini risasi
jinsi
ya kujikinga na madhara ya madini ya Risasi
·
ni vema jamii ikajitahidi kuzuia vumbi la
aina yoyote
·
katika maandalizi ya chakula ni vyema kuandaa
lishe kwa kutumia maji baridi
·
ni vema kunawa mikono kabla na baada kula
·
kutenganisha
shughuli za upakaji rangi na uwepo wa watoto na kupaka rangi zisizo na madini risasi
·
ni vema kuwapima watoto wingi wa madini
chuma,hususani watoto walio chini ya miaka 2
·
kusimamia usafi wa watoto kila watokapo
kucheza
kuelekea october23-29
Mimi na wewe ni jukumu letu kuwalinda watoto wetu dhidi
ya matumizi ya risasi mwilini
nawasilisha
0713390903
Post a Comment