Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MANJI NA WAZEE SASA NI VITA JANGWANI, AKILIMALI KUONGOZA UPINZANI

Mzee Ibrahimu Akilimali
Na: Imani Kelvin Mbaga 
    
  Kamati maalum ya muafaka ya wazee wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, leo imetanagaza kutotambua taarifa za mchakato wa kukodisha timu hiyo kwa kampuni ijulikanayo kama Yanga yetu Ltd inayoongozwa na mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo Yusuph Mehboob Manji.
    Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo leo jijini Dar es salaam, katibu wa kamati hiyo mzee Ibrahim Akilimali, amesema wazee wa klabu hiyo wanapinga mpango wa mwenyekiti wao kutaka kuikodisha timu yao na kusema kuwa mchakato mzima ni batili kwa kuwa haukupata ridhaa ya vikao halali vya klabu hiyo na kwamba hakuna utaratibu wa kukodisha timu popote duniani.
    "Yanga ni klabu kubwa na yenye historia iliyotukuka, hivyo haiezi kukodishwa. Manji ametumia njia ya mabavu na kutaka kukodishiwa timu klabu yetu jambo ambalo hatutakubali hata siku moja" Alisema Akilimali.
   Aidha mzee Akilimali alisema kuwa mwenyekiti wao alikuwa ni mmoja kati ya watu waliochangia kuileta pamoja klabu hiyo baada ya kupita kwenye mgogoro mkubwa mwaka 2000 hadi 2006 baada ya wanachama wa klabu hiyo kugawanyika katika makundi matatu aliyoyataja kuwa ni Yanga kampuni,Yanga asili na Yanga akademia, mgogoro uliohitimishwa mwaka 2006 kwa kutiwa saini makubaliano maalumu yaliyozaa Yanga Sc kama klabu ya michezo na Yanga Cooperatin Ltd itakayoshughulikia masuala ya kibiashara ambapo klabu ingekuwa na hisa za 51% huku wanachama wakipewa 49%.
    Naye Mohamedi Msumi aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya Yanga mkoa wa Dar es salaam akiongea
Mzee Akilimali akisisitiza jambo habari maelezo
                                                                 katika mkutano huo amesema mchakato wa kukodisha klabu hiyo haukufuata taratibu za kikatiba wala kujali sheria na katba ya nchi kwa jumla.
Msumi ameeleza kuwa ili taratibu zionekane kufuatwa ni lazima suala hilo lijadiliwe na kamati tendaji kabla ya kupelekwa kwenye bodi halali ya wadhmini kitu ambacho hakikufanyika. Msumi pia  alisema baraza la wadhamini linalotajwa kutumiwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji siyo bodi halali ya wadhamini wa klabu hiyo linalotambuliwa na taasisi ya RITA ambapo amesema kuwa baada ya muafaka uliofikiwa mwaka 2006 majina saba ya bodi ya wadhamini ya muda yaliwasilishwa na kupitishwa na taasisi hiyo ambapo ametaja majina hayo kuwa ni George Mkuchika, Fatma Karume, Ami Ramadhani, Juma Mwombelo, Juma Kambi, Mohamed Abeid Abeid na Francis Kifukwe, hivyo jina la Jabir Katundu halikuwapo katika orodha hiyo.
   "Mwenyekiti wetu anavunja katiba kwa makusudi huku akiwa anajua analolifanya na anasaidiwa na Francis Kifukwe na lengo lao ni kuyafanya hayo waliyoyaficha kwa makusudi, huku wakitumia njia za uongo kuwadanganya watanzania" Alisema Msumi.
    Hata hivyo wazee hao hawakuwa tayari kuweka wazi iwapo watahudhuria kwenye mkutano wa dharura ulioitishwa na mwnyekiti wa klabu hiyo siku ya Jumapili ya tar 23 Oct kujadiliana juu mambo mbalimbali ikiwemo suala la kukodishwa kwa klabu hiyo licha ya kuweka wazi azma yao ya kufungua mashtaka dhidi ya maamuzi yoyote ya mkutano huo yatakayosaidia kukamilisha mchakato wa kukodishwa kwa klabu hiyo.
    Tayari serikali imetoa msimamo wake juu ya suala hilo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kusema kuwa haitambui mchakato huo kutokana na kukiuka katiba ya klabu pamoja na sheria za nchi.



No comments

Powered by Blogger.