Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

VUMBI LA LIGI KUU TANZANIA BARA LITATIMKA KESHO JUMATANO NA ALHAMISI.

 LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA

Ratiba:

Jumatano Oktoba 19

Azam FC v Mtibwa Sugar [Kuanza Saa 1 Usiku]

Ruvu Shooting v Mwadui FC

Ndanda FC v Mbeya City

Tanzania Prisons v Stand United

Toto Africans v Yanga

African Lyon v Maji Maji FC

Ligi Kuu ya soka Tanzania bara, itaendelea Jumatano kwa Mechi 6 huku Mechi moja ikichezwa Usiku.

Kwenye Mechi hizo, Mabingwa Watetezi Yanga wapo huko CCM Kirumba Mwanza kucheza na Wapwa zao Toto Africans.

Yanga, ambao Juzi walitoka 0-0 na Azam FC, wapo Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 15 kwa Mechi 8 wakati Vinara ni Simba wenye Pointi 23 kwa Mechi 9.

Mechi nyingine za Jumatano ni za huko Mlandizi kati ya Ruvu Shooting na Mwadui FC wakati huko Nangwanda, Mtwara, Ndanda FC watacheza na Mbeya City na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Stand United ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 20 kwa Mechi 10.

Jijini Dar es Salaam zipo Mechi mbili na moja itaanza Saa 10 huko Uhuru kati ya African Lyon na Maji Maji FC wakati huko Chamazi, Azam Complex, Wenyeji VPL-OKT18Azam FC watacheza na Mtibwa Sugar kwenye Mechi itakayoanza Saa 1 Usiku.

Mechi hii itaanza Saa 1 Usiku kwa ridhaa ya TFF kutokana na maombi ya Azam TV kuonyesha Mechi nyingi Laivu Siku hiyo ya Jumatano.

VPL itaendelea tena Alhamisi kwa Mechi 2 kati ya Simba na Mbao FC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na huko Mlandizi ni kati ya JKT Ruvu na Kagera Sugar.


YANGA - Mechi zao:

Okt 19 Toto African v Yanga

Okt 22 Kagera Sugar v Yanga

Okt 26 Yanga v JKT Ruvu

Okt 29 Yanga v Mbao FC

SIMBA - Mechi zao:

Okt 20 Simba v Mbao FC

Okt 23 Simba v Toto African

Okt 29 Mwadui v Simba

Nov 2 Stand United v Simba

 LIGI KUU
Ratiba:

Alhamisi Oktoba 20

Simba v Mbao FC

JKT Ruvu v Kagera Sugar

No comments

Powered by Blogger.