Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

DAKIKA ZA LALA SALAMA TRUMP NA HILLARY CLINTON


Hillary Clinton na Donald Trump wamefanya mikutano ya dakika za mwisho mwisho kuwahimiza raia wa Marekani wawapigie kura zikiwa zimesalia saa chache kabla ya uchaguzi kufanyika, Wote wawili wamefanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya kushindaniwa ya Carolina Kaskazini, Pennsylvania na Michigan, Clinton amewahimiza wapiga kura kuunga mkono kuwepo kwa “Marekani yenye matumaini, inayojumuisha wote na yenye ukarimu”.

Trump naye amewaambia wafuasi wake kwamba wana “fursa nzuri ya kuvunja mfumo mbovu na usio na maadili”. Kura za maoni zinaonesha Bi Clinton wa chama cha Democratic akiwa asilimia nne mbele ya mpinzani wake Bw Trump wa chama cha Republican.

Wapiga kura wengi kuliko awali, zaidi ya 46 milioni, tayari wamepiga kura za mapema, Kuna ishara za wapiga kura wa asili ya Kihispania (Latino/Mexico) kujitoleza kwa wingi, jambo ambalo wengi wanaamini litamfaa Clinton.

Uchaguzi mkuu unafanyika baada ya kampeni kali ambapo wapiga kura walirushiana matusi na kila mmoja alikabiliwa na kashfa, Kwenye hafla Philadelphia, Pennsylvania, Bi Clinton ameungana na nyota Bruce Springsteen na Jon Bon Jovi jukwaani pamoja na mumewe Bill, Rais Obama na mkewe Michelle

Obama amewataka wapiga kura kukataa kutawaliwa na woga na badala yake waamue kukumbatia matumaini, Mkutano wa mwisho wa kampeni wa Bi Clinton ulikuwa Raleigh, Carolina Kaskazini, ambao angemshirikisha Lady Gaga, Awali, alisema kwenye mahojiano redioni kwamba akishinda atampigia simu Bw Trump na kwamba anatumai mgombea huyo wa chama cha Republican anaweza “kutekeleza mchango muhimu” katika kuunganisha tena taifa hilo.

Trump, kwenye mkutano wake wa kampeni mjini Scranton katika jimbo hilo alisisitiza kwamba kampeni yake imekuwa ikiimarika, Mkutano wake wa mwisho ulikuwa Grand Rapids, Michigan, Awali, aliwaambia wafuasi wake jimbo la Florida kwamba yeye “si mwanasiasa” na kwamba anawajali wao pekee.

No comments

Powered by Blogger.