DIRISHA DOGO KUFUNGULIWA KATIKATI YA NOVEMBA
Na Imani Kelvin Mbaga
Ligi kuu ya
kandanda Tanzania bara “VPL” inatarajia kukamilisha mzunguko wa kwanza tar 12
Nov mwaka huu na kuruhusu milango ya dirisha dogo la usajili kuanza ili kuwapa
fursa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza pamoja na ligi
daraja la pili kufanya usajili wa wachezaji kuziba nafasi zilizopo na
kuimarisha vikosi vyao.
![]() |
Alfred Lucas msemaji wa TFF |
Kwa mujibu
wa taarifa ya shirikisho la soka nchini TFF zilizotolewa leo jijini Dar es
salaam na msemaji wake Alfred Lucas zilisema kuwa dirisha dogo la usajili nchini litadumu kwa mwezi mmoja kuanzia tar 15 ya mwezi Novemba hadi tar
15 ya mwezi Desemba mwaka huu.
“tunaviasa
vilabu vyote kulitumia vizuri dirisha dogo la usajili ili kuimarisha vikosi
vyao, tena vifanye hivyo kwa umakini ili kuhakikisha kuwa wanapata wachezaji
bora kuziba nafasi zilizopo kwenye vilabu vyao” Alisema Lucas
Wakati
huohuo shirikisho limesema kuwa linaridhishwa na mwenendo wa ligi hiyo hadi
sasa na kwamba watahakikisha mzunguko wa pili unakuwa bora usio na malalamiko
mengi.
Ligi hiyo
inatarajiwa kuendelea tena kesho katika jumla ya viwanja sita
Majimaji –
Ruvu Stars
Mbeya City-
Young Africans
Ndanda-Tanzania
Prisons
Ruvu
Shooting-African Lyon
Stand
U-Simba
Toto
Africans-Azam fc
Bado Simba
inaongoza ligi hiyo kwa pointi 32 huku wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga ambao
wana pointi 27.
Post a Comment