KESI YA "KESSY" BADO NI "KIZUNGUMKUTI"
Na: Imani Kelvin Mbaga
Hatima ya
mchezaji Hassan “kessy” Ramadhani inatarajia kujulikana tar 3 Novemba baada ya kikao cha mariadhiano kati ya Simba
na Yanga chini ya msuluhishi huru,
kiongozi wa zamani wa kilichokuwa chama cha soka nchini “FAT”, Said
El-Maamri.
![]() |
Hassan "Kessy" Ramadhan |
Akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo msemaji wa shirikisho la soka
nchini Tanzania (TFF) Alfred Lucas, alisema
baada ya kesi hiyo kuwasilishwa kwenye kamati ya sheria maadili na hadhi
za wachezaji iliamuliwa kuwa vilabu
husika vikae na kujadiliana juu ya suala hilo chini ya msimamizi huru na kwamba
tar iliyopangwa ilikuwa ni tar 29 mwezi uliopita.
Hata hivyo
suala hilo halikumzungumzwa siku hiyo kutokana na udhuru aliokuwa nao mwanasheria
wa klabu ya Yanga Alex Mgongolwa, hivyo iliamuliwa shauri hilo liendelee tar 3
ya mwezi huu.
Hata hivyo
shirikisho limevitahadharisha vilabu hivyo kukubaliana na visipofanya hivyo
basi litarudishwa kwenye kamati husika na kuamuliwa kwa mujibu wa sheria.
Hassan “Kessy”
alisajiliwa na klabu ya Yanga akitokea kwa mahasimu wao wa jadi Simba Sc ya
jijini Dar es salaam huku Yanga wakidai kuwa alikuwa mchezaji huru jambo ambalo limekanushwa mara kadhaa na
klabu yake ya zamani Simba.
Suala hilo
lilifikishwa kwenye kamati ya ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji ambako
mchezaji aliruhusiwa kuendelea kucheza soka ili kulinda kipaji chake wakati
suala lake likiwa linashughulikiwa na vilabu vyake.
Post a Comment