SERENGETI BOYS KWENDA KOREA MWEZI HUU
Na Imani Kelvin Mbaga
Timu ya
Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti boys inatarajia kuingia
kambini hivi karibunui ili kujiandaa na michuano ya kirafiki ya kimataifa itakayo
fanyika Korea ya kusini kuanzia tar 9 mwezi huu.
![]() |
Msemaji wa TFF Alfred Lucas |
Shirikisho
la soka nchini TFF limesema vijana hao wataendelea kutunzwa na kwamba ahadi ya
Rais wa shirikisho hilo Jamali Malinzi kwa vijana hao kuendelea kuwa timu za
taifa na kupewa msaada wowote watakaouhitaji ili kufikia malengo ya shirikisho
Msemaji wa
TFF Alfred Lucas alisema kocha wa timu hiyo Bakari Shime Nyundo amewasili leo
kutoka mkoa Tanga na kwamba kambi hiyo itaanza hivi karibuni kabla vijana hao
hawajaondoka kuelekea huko Korea ya Kusini.
Lucas pia ameeleeza
kuwa timu ya taifa ya wakubwa yaani Taifa Stars itaitwa hivi karibuni ili
kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe utakaochezwa
katika wiki ya shirikisho la soka ulimwenguni FIFA .
“Zimbabwe
wameonyesha nia ya kucheza nasi katika wiki ya michezo ya FIFA na baada ya
kutuandikia barua ya kuomba kucheza na timu yetu tumekubali ili tukifanya
vizuri tuweze kupanda katika nafasi za ubora za msimamo wa FIFA” Alisema Lucas
Kutokana na
mchezo huo kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa, anatarajiwa
kuita kikosi chake siku yoyote ili kuingia kambini kujiandaa na mechi hiyo
muhimu.
Post a Comment