Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MABALOZI WA USALAMA BARABARANI WAJA NA ABIRIA PAZA SAUTI

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani  mhe, Yusuph Masauni akizindua kampeni ya usalama barabarani



Na; Imani Kelvin Mbaga,Dar es salaam.

Taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama, mabalozi wa usalama barabarani imezindua kampeni maalumu ijulikanayo kama “abiria paza sauti” kwa lengo la kupunguza ajali za makusudi zinazosababishwa na madereva na watumiaji wengine wa barabara, kwa kuwataka abiria kutonyamazia vitendo vyote vinavyosababisha ajali.

Akizungumza na wadau wa usalama barabarani katika uzinduzi huo, mgeni rasmi, mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani taifa ambaye pia ni naibu waziri wa mambo ya ndani, mhe. Yusuph Masauni, alipongeza kampeni hiyo na walioibuni, na kusema kuwa serikali itakuwa nao bega kwa bega katika utekelezaji wa kampeni hiyo.

“Nimefurahi sana leo kualikwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampni hii muhimu kwa usalama wa abiria na mali zao. Tumekuwa tukipambana na suala hili kwa muda mrefu sasa na ninaahidi kwa niaba ya serikali kutoa ushirikiano ili kukomesha ajali barabarani” Alisema Masauni.

Naye kamanda wa kikosi cha polisi wa usalama barabani DCP, Mohamed Mpinga, alisema kuwa hii ni matokeo ya jitihada za miaka mingi za kudhibiti ajali na kuhahakisha usalama wa abiria unazingatiwa, juhudi zilizoanzia kwenye mitandao ya kijamii hadi kuzaa taasisi hiyo, ambayo ina mikakati ya kuwashirikisha abiria katika kudhiti usalama wao.

“Miaka iliyopita ytulikuwa na makundi mawili ambayo yaliundwa kwa lengo la kupambana na ajali na lingine kuwakwepa polisi lakini kwa juhudi kubwa tulifanikiwa kuyaunganisha makundi hayo na kupata mabalozi wa usalama barabarani” Alisema Kamanda Mpinga.

Awali wakati wa risala, katibu wa taasisi hiyo, Asina Omary, alisema taasisi yao ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imesajiliwa rasmi kama taasisi isiyo zalisha faida, na kwamba ni muungano wa wadau na wakereketwa wa usalama barabarani ambao kwa pamoja wameamua kutoa elimu kwa madereva na abiria ili kudhibiti ajali kwa kiasi kikubwa.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na taasisi mbalimbali, wadau wa usafiri na wananchi kwa jumla na ulifanyika ndani ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi kilichopo Ubungo jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.