Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MECHI YA MWISHO MZUNGUKO WA KWANZA YANGA YAIPANDIA SIMBA KILELENI


kikosi cha Yanga Sc

Na: Imani Kelvin Mbaga

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara, Yanga Sc leo wamefanikiwa kupunguza pengo la pointi lililokuwapo kati yao na vinara wa ligi hiyo Simba Sc hadi kufikia pointi mbili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Ruvu walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza dakika saba tu toka mchezo huo uanze likifungwa na Abdallah Hamiss, huku wakionekana kutoa upinzani kwa Yanga hasa dakika 20 za mwanzo, kabla Yanga hawajageuza mchezo kwa kutumia viungo na wachezaji wao wa pembeni Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao umiliki na kasi yao ya mchezo viliwalazimisha Ruvu kurudi nyuma na kukaribisha mashambulizi langoni mwao.

Simon Msuva dakika ya 32 aliwainua mashabiki wa Yanga vitini mwao baada ya kusawazisha goli na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko timu zote zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

Kipindi cha pili Yanga walionekana kucheza kwa kasi hasa kupitia upande wao wa kulia ambako Msuva na Kessy walionekana kucheza vizuri sana na endapo washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini basi wangewza kuibuka na ushindi mnono wa magoli mengi.

Dakika ya 62 Haruna Niyonzima alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Donald Ngoma kuifungia Yanga Yanga goli la pili na la ushindi. Hata hivyo mshmbuliaji Amiss Tambwe alikosa mabao kadhaa ya wazi kwa ama kupaisha mpira juu au kuishia mikononi mwa mlinda mlago wa Ruvu Shooting,hali kadhalika Obrey Chirwa wa Yanga pia alikosa mabao kadhaa.

Licha ya kucheza vizuri mwanzo wa mchezo huo Ruvu walionekana kulemewa sana hasa mwishoni mwa kipindi cha kwanza na mwanzoni mwa kipindi cha pili ambapo walinekna kucheza zaidi katika eneo lao jambo ambalo lilikuwa la hatari kwao.

Ruvu pia walonyesha kushindwa kuzitumia nafasi chache walizotengeneza katika mchezo wa leo na hivyo hadi mwisho kujikuta wakiangukia pua.

Yanga walionekana kutulia hata pale walipotangulia kufungwa goli mla mapema walicheza kwa maelewano makubwa hasa katika safu ya kiungo huku kivutio kikubwa kikiwa  mchezaji Hassan Kessy aliyeonekana kucheza vizuri zaidi katika nafasi ya mlizi wa kulia ambako Juma Abdul aliyezoeleweka na kuaminiwa kwa muda mrefu akiwa majeruhi.

Goli la Haruna Niyonzima ni goli la 31 kwa Yanga na linaifanya kuwa klabu iliyo funga magoli mengi zaidi katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambo umehitimishwa leo kwa mechi hiyo.

Mzunguko wa pli unatarjia kuanza tena katikati ya mwezi wa Desemba huku dirisha dogo la usajili likifunguliwa tarehe 15 mwezi huu.

Kwa matokeo hayo hayo sasa Yanga wanashika nafasi ya pili huku wakiwa pointi 2 tu nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba Sc ambao wiki moja iliyopita walikuwa nyuma yao kwa pointi 8 kiasi cha kuwafanya baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuanza kukata tamaa ya ubingwa

No comments

Powered by Blogger.