tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25
Home/
Unlabelled
/KARIBU KATIKA STORY TATU ZILIZONASWA NA EVERNING SATELITE YA MAMBO BAYANA NI PAMOJA NA MKE WA RAIS MAGUFULI MAMA JANETH ALAZWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
KARIBU KATIKA STORY TATU ZILIZONASWA NA EVERNING SATELITE YA MAMBO BAYANA NI PAMOJA NA MKE WA RAIS MAGUFULI MAMA JANETH ALAZWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Story namba moja ni kuugua kwa mke wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mama Janeth
Ikulu imetoa picha ya Rais Magufuli akimjulia hali katika wodi ya Sewa Haji.
Hata hivyo, haijasema anaugua wapi.
Novemba
mwaka jana, siku chache baada ya kuapishwa hospitali hiyo ni miongoni
mwa taasisi za serikali ambapo Rais Magufuli alifanya ziara ya
kushtukiza.
Alisema alisikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini.
Alidha,
alipata hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi
na mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN
zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi kadha.
Alibadilisha usimamizi wa hospitali hiyo.
Taarifa
ya ikulu inasema leo, alipokuwa anamjulia hali mkewe, pamoja na mke wa
balozi na waziri mstaafu wa Tanzania Omar Ramadhan Mapuri, wagonjwa
waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji wamemshukuru "kwa hatua
zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili na
wamebainisha kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, pia
wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi."
Story namba mbili katika mastory kibao ya Mambo bayana leo ni hii hapa inayohusu Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka kutoka nchini marekani atoa tamko baada ya ushindi wa Trump
Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka,
anasema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa
rais.
Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angeirarua green Card yake, ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika.
Soyinka alitoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza.
Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump.
Soyinka alishinda tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hilo.
Na story ya mwisho ambayo imenaswa na evining Satelite ya mambo bayana na ipo clear kukufikishia habari inamuhusu muhubiri maharufu kutoka nchini Nigeri, TB Joshua arejesha utabiri wa ushindi wa Clinton Facebook
Utabiri kutoka kwa mhubiri raia wa Nigeria TB Joshua kuwa Hillary
Clinton angeshinda urais wa Marekani, umerejeshwa tena baada ujumbe huo
kufutwa kutoka mtandao wa Facebook.
Kulingana na barua pepe iliyotumwa na idara ya mitandao ya
kanisa la TBJMinistries ilisema kuwa , "ujumbe huo uliondolewa kimakosa
na sasa umereswa kwa kuwa hiyo si sera yetu."
"Siku kumi zilizopita nilimuona rais wa Marekania akishinda kwa kura chache, yule niliyemuona ni mwanamke," ujumbe huo ulisema.
TB
Joshua alikejeliwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakati watu
walitambua kuwa ujumbe huo ulikuwa umefutwa, licha ya wafuasi wake
wengi katika mitandao ya kijamii bado kumtaja kuwa nabii.
Usikose kusikiliza kipindi cha mambo bayana kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa saa kumi kamili za jioni mpaka kumi na mbili za jioni, tune tanganyikafm online radio.
Post a Comment