Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MOTO WATEKETEZA GHALA LA SABA GENERAL ENTERPRISES LIMITED.



Na Joseph Peter Dar es Salaam.

Moto mkubwa umezuka katika Ghala la Saba General Enterprises Limited linalohifadhi vipuri vya baiskeli,piki piki,Magari pamoja na Magurudumu ya vifaa hivyo kilichopo Mikocheni karibu na chuo Kikuu cha Tumaini Jijini Dar es Salaam majira ya saa 7:02 Mchana na kuteketeza mali zote zilizopo ndani ya ghala hilo.

Akitoa taarifa za awali juu ya moto huo eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa kindondoni Kamishna msaidizi wa polisi{ACP} Suzan Kaganda amesema kuwa wamepokea taarifa kuwa ghala hilo linawaka moto hivyo wakawasiliana na wenzao kikosi cha kuzima moto ili kuweza kufika haraka eneo la tukio kwa ajili ya kupambana kuuzima moto huo.

"moto kama mnavyouona tulipokea taarifa kupitia wenzetu kwamba hili ghala la Saba General Enterprises linawaka moto na mara moja tuliwasiliana na wenzetu wa fire.....kama mnavyoona shughuli inaendelea ya kuzima siwezi kuzungumza mengi hatujajua chanzo  lakini mpaka dakika hii watu wote waliokuwa kiwandani wametolewa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, kampuni binafsi, Ultimate security,Night support,wamiliki wa Viwanda pamoja na jeshi la polisi wanashirikiana ili kuuzima moto huo" alisema Kaganda.

Aidha kamanda Kaganda amesema kuwa moto huo umezuka eneo hilo ambapo nyuma ya Ghala hilo kuna kiwanda kingine cha kutengeneza tisue paper  hivyo akawaomba waandishi wa habari kuendelea kufuatilia tukio hilo huku wakiendelea kupambana kuuzima moto huo kwanza na  mara baada ya kufanikiwa  kuuzima watatoa taarifa rasmi.

Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Salum Amesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambayo ilianzia ndani ya jengo hilo na kusambaa katika maeneo mengine  na wakaanza juhudi za kuhamisha baadhi ya vitu kama magari na vinginevyo kwa lengo la kuvinusuru.

Taarifa za chanzo cha moto huo ikiwemo thamani ya mali zilizoteketea zitakujia kadri tunavyozidi kuendelea kufuatilia kwa undani zaidi.
 Baadhi ya Magari ya Zimamoto wakiendelea kupambana na moto huo.

 Baadhi ya wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo huku wakiwa wamedhibitiwa na askari  jeshi la polisi.
Askari wa jeshi la zimamoto wakiwa katika harakati za kuuzima moto huo.

 Juhudi zikiendelea ili kuuzima moto huo
 Sehemu ya mbele ya Ghala la Saba General Enterprises Limited likiendelea kuwaka moto
Magari ya kikosi cha zimamoto yakiwa katika eneo la tukio

No comments

Powered by Blogger.