Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MFAHAMU MSANII WA KIZAZI KIPYA "ROBINET"


Na Joseph Peter,Dar es Salaam.
Historia ya muziki wa kizazi kipya au Bongo Flava kama unavyojulikana miongoni mwa wengi  una historia ndefu kiasi kwamba  leo hii wengi hatukumbuki tena hata muziki huu ambao  umetokea kuwa kipenzi cha wengi ulianzaje,ukapitia hatua na harakati gani mpaka kufikia hapa ulipo leo.

Ukirudi nyuma na kuangalia historia ya muziki wa Bongo Flava kwa hapa nyumbani Tanzania miaka kadhaa iliyopita ilikuwa ni moja kati ya muziki ambao haukupatwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na baadhi ya watu Kutokana na Maudhui yake Kuwachanganya walio wengi pamoja na mtindo wa uimbaji wake na wahusika wenyewe kuwa ni rika fulani ya vijana ambao walionekana ni wahuni.

Lakini kila kitu huwa kinakuwa na changamoto nyingi sana kikubwa ni uvumilivu ndicho kitu pekee kilichojidhihirisha katika mapito ya muziki huu ambapo kwa sasa imekuwa ni ajira inayowapa wasanii fursa ya kujikwamua kiuchumi pia jamii imefikia hatua ya kuelewa nini kinachofanyika pamoja na mchango wake katika Kuleta maendeleo kupitia tasnia hii.

Sasa leo namleta kwako msanii wa kizazi kipya ambaye ni  kati ya vijana wanaotumia nafasi hii kutafuta njia ya kuleta mabadiliko makubwa lakini pia kutengeza ajira, Anaitwa Robert William jina la sanaa ni Robinet ambaye amezaliwa wilayani Geita zamani mkoa wa Mwanza {sasa Geita mkoa} mnamo tarehe 15 mwezi juni mwaka 1988.

Maisha yake kwa sasa yapo Sinza-Kumekucha Jijini Dar es Salaam  Anajishughulisha na ujasiriamali, kwa ufupi safari yake kimuziki ilianza mwaka 2004 akiwa amefanya baadhi ya kazi katika mitindo tofauti ya uimbaji kama vile Rap na aliweza kurekodi nyimbo kama Ujio wa Vitisho,Take care na One key For one lock kipindi hicho akijiita Sneb na baadae akabadilisha jina na kujiita Desturi ambapo alifanikiwa kurekodi wimbo uitwao Sorry Lord Version 1 uliotoka mwezi oktoba mwaka 2015 kisha akarekodi cover ya  wimbo uitwao Ndi ndi ndi wa Msanii Lady Jay Dee remix aliomshirikisha Msanii huyo wa kike anayefanya vizuri kimuziki na rekodi hii ilitoka mwezi june Mwaka 2016.

Mwaka 2013 akatoa wimbo unaitwa Darasa Huru aliomshirikisha Soprano uliorekodiwa katika studio za Amba Records jijini Dar es Salaam, pia baadae akatoa rekodi nyingine ikiwa ni marudio ya wimbo Sorry Lord Sehemu ya pili aliomshirikisha msanii Dan Love ukihusisha ujuzi wa wazalishaji wawili tofauti P Funk Majani wa Bongo Records aliyetengeneza Mdundo pamoja na studio ya Paradize iliyofanya sauti{vocal} na Mixing mnamo mwezi Septemba mwaka 2016 hapa akitumia jina la Robinet ambalo ndilo linalomtambulisha kwa sasa katika sanaa ya muziki huu.

Sorry Lord ni wimbo unaozungumzia maisha ya kila siku katika jamii yetu kwamba kuna wakati baadhi ya watu huwa tunajisahau kwa kufanya dhambi na makosa mbali mbali kama vile uzinzi hivyo inatupasa kukiri na kuomba juu ya aliyetuumba,Mahusiano yana mipaka lakini kuna baadhi ya watu wanashindwa kuwa na uvumilivu na kujikuta wakifanya uzinzi sasa inafika wakati unatakiwa kuachana na tabia kama hizo kwa kumrudia bwana na hiki ndicho kinachozungumziwa na msanii Robinet.

Ili kufika mbali inahitajika ushirikiano na nguvu kubwa kutoka kwa jamii kwa hiyo anaomba support yako pia kaa mkao wa kula kwa wimbo mwingine ambao utatoka hivi punde unaoitwa This Life unaotegemewa kutoka mwezi Disemba mwaka 2016.

Lengo kubwa ni kutaka kukuza na kuinua vipaji vya vijana kupitia sanaa hii na kuifanya kuwa ni ajira rasmi inayoweza kumkomboa kijana wa Kitanzania hata katika hatua za kimataifa na mwisho katika kuzungumza nae ameweka bayana kuwa ana mpango wa kumili Lebo yake pamoja na kutengeza pesa.

Kama una maoni au ushauri  Kwa Msanii Robinet usisite tuma ujumbe au unaweza kupiga simu yake ya mkoni namba 0718978045.

No comments

Powered by Blogger.