Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

MSAJILI AFUTA VYAMA VITATU VYA SIASA

                                                                                                           Na: Imani Kelvin Mbaga

Jaji Francis Mutungi
Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, mh, Jaji Francis Mutungi, ametangaza kuvifuta vyama vitatu vya siasa kwa sababu mbalimbali kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa  namba 5 kifungu cha 19 ya mwaka 1992 inayompa mamlaka msajili kufanya hivyo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo, Jaji Mutungi alisema katika zoezi la uhakiki lililofanyika la uhakiki, vyama vilivyofutiwa usajili vilibainika kuwa vimepoteza sifan ya usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Vyama Vya Siasa.
Vyama vilivyokumbwa na adhabu hiyo ni pamoja na, Chama Cha Haki Na Ustawi (CHAUSTA), kilichopata usajili wa kudumu tarehe 15 Novemba 2001, kiongozi wake akiwa James Mapalala aliyekuwa mwenyekiti huku Lameck Mgimwa akiwa katibu, The African Progressive Party (APPT-Maendeleo), kilichopata usajili wa kudumu tarehe 4 March 2003 na kiongozi wake alikuwa Peter Kuga Mziray kama Rais mtendaji wa Taifa na Nziame Samwel katibu mkuu na chama cha Jahazi Asilia kilichopata usajili wa kudumu tarehe 17 Novemba 2004 na kilikuwa kinaongozwa na Kasimu Bakari Ally mwenyekiti huku katibu wake akiwa Mtumweni Jabir Seif.
Akizitaja sababu zilizosababisha kufutwa vyama hivyo, Jaji Mutungi alisema, kutokuwa na ofisi ya Chama Tanzania bara na Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 10(d), kutokuwa na wanachama Zanzubar kwa mujibu wa kifungu cha 10(b), kushindwa kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya chama kwa mujibu wa kifungu cha 14(1)(i), kushindwa kuwasilisha hesabu zake zikaguliwe kwa mkaguzimkuu wa hesabu za serikali ili zikaguliwe kwa mujibu wa kifungu cha 14(1)(b)(i), kushindwa kuwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa tamko la orodha ya mali za chama kwa mujibu wa kifungu cha 14(1)(b)(ii) au kushindwa kutekeleza matakwa ya kifungu cha 15(1) kwamba mapato yote ya chama yawekwe kwenye akaunti ya chama.
Msajili huyo pia amewakumbusha wanachama wa vyama hivyo vilivyofutwa kutofanya shughuli yoyote ya kisiasa kwa kutumia jina la chama cha siasa kilichofutwa kwakuwa kufanya hivyo itakuwa ni kuvunja sheria ya vyama vya siasa kifungu cha 7(3) inayotaka taasisi yoyote inayofanya kazi za kisiasa iwe imesajiliwa kwa mujibu wa sheria hiyo

No comments

Powered by Blogger.