Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

SIMBA YALALA "DORO" TENA, AZAM YAZINDUKIA KWA MWADUI

kikosi cha Simba
Na; Imani Kelvin Mbaga

Vinara wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara Simba Sc kwa mara ya pili mfululizo walijikuta wakiangukia pua kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo uliokuwa muhimu kwao kushinda ili kujiimarisha kileleni kabla ligi hiyo haijakwenda mapumziko kusubiri mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi Desemba, Simba walijikuta wakizidiwa maarifa na wapinzani wao Prisons ambao kipindi cha pili cha mchezo huo walionekana kucheza vizuri zaidi.
Jamal Mnyate aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 43 kwa kichwa akiunganisha mpira uliopigwa na winga machachari wa klabu hiyo Shiza Kichuya. Kwa jumla kipindi cha kwanza Simba walionekana kuwa bora zaidi katika eneo la kati ya uwanja pakitawaliwa zaidi na Jonas Mkude, Muzamiru Yassin, Jamal Mnyante na Shiza Kichuya.
Hata hivyo baada ya mapumziko Tanzania Prisons walionekana kubadilika na kucheza vizuri kwa kutumia mipira mirefu huku wakionekana kuwa vizuri kwenye fiziki na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 47 baada ya Victor Hangaya kuisawazishia timu hiyo goli kwa kichwa kuunganisha mpira wa Salum Kimenya, kabla ya kuifunguia goli la ushindi katika dakika ya 63.
Licha ya Simba kuonyesha juhudi ya kutaka kurejesha goli hilo Prisons walionekana kucheza kwa nidhamu kubwa ya ukabaji na hadi mwisho wa mchezo waliondoka uwanjani kifua mbele kwa mabao 2-1.
Wakati  Simba wakipoteza mechi hiyo wenzao wana lambalamba waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 mbale ya Mwadui fc ya huko mkoani Shinyanga katika mchezo uliochezwa Mwadui Complex.
Mwadui na Azam ni timu ambazo msimu huu hazifanyi vizuri ukilinganisha na msimu uliopita hata hivyo katika mchezo wa leo Mwadui wameendelea kuonyesha udhaifu mkubwa katika ukabaji na nidham ya mchezo kwa jumla kitu kinachotishia kubaki kwao kwenye ligi ya mwaka huu.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja kati ya Yanga ya jijini Dar es salaam itakapo wakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka mkoani Pwani, mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na matokeo ya mechi za leo.
Baada ya mchezo huo wa kesho ligi hiyo itasimama kwa muda wa mwezi mmoja hadi katikati ya mwezi Desemba huku vilabu vikipata fursa ya kufanya usajili katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo linalotarajiwa kuwa wazi kwa mwezi mzima toka tar 15 mwezi Novemba hadi tar 15 Desemba.

No comments

Powered by Blogger.