Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

OFISI YA WAZIRI MKUU YAPOKEA MIFUKO 1000 YA SERUJI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MAAFA KAGERA.

HABARI KATIKA PICHA, ZIKIONYESHA MATUKIO MBALIMBALI YA MAKABIDHIANO YA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI KAGERA (picha kwa hisani ya ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Amsons-Camel Bw. Salim A.Salim baada ya kukabidhi msaada wa Mifuko 1000 ya Seruji kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi la Kagera Novemba 09, 2016 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim (kushoto) akitoa maelezo ya msaada wa mifuko 1000 ya Seruji kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) walipofika katika Ofisi yake Dar es Salaam Novemba 09, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika zoezi la makabidhiano ya mifuko 1000 ya seruji kwa ajili ya waathirika wa maafa mkoani Kagera kutoka Kampuni ya CAMEL katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (katikati) akipeana mkono wa shukrani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim wakati wa kuwasilisha msaada wao wa mifuko 1000 ya Seruji kwa waathirika wa maafa Kagera, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Amsons-Camal Bw. Ghalib H. Ghalib. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments

Powered by Blogger.