RAIS MAGUFULI APIGILIA MSUMARI WA MWISHO MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI
“Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri sana kwa nchi hii,
wale wanaoandika vizuri na hata wanaoongeza chumvi nawapenda wote. Mfano ndugu
yangu kipanya anayenichora kwenye katuni saa zingine najitazama kwenye kioo
kama nna kichwa kama vile anavyonichora … lakini yote kwa yote nipo pamoja
nanyi na wala msiwe na wasiwasi i love you all”.MAGUFULI
Hayo ni maneno yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema leo alipokutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo tathimini ya utawala wake tangu akae madarakani ambapo kesho Novemba 5 anatimiza mwaka mmoja tangu kuapishwa kwake.

Alipoulizwa na Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari (MOAT) juu ya sheria zinazohusiana na tasnia ya habari kuwasilishwa
bungeni kwa hati ya dhadhura kama ilivyokuwa kwa Sheria ya Makosa ya Mitandao
(Cyber Crime Act 2015), Sheria ya Takwimu na Sheria ya Muswaada wa Huduma za
Vyombo vya Habari ambayo itataanza kujadiliwa hapo kesho huku wadau mbalimbali wakitaka
kuongezewa muda ili wapate fursa ya kujadili kwa kina Rais Magufuli amesema
wadau hao walipaswa kujadili mapema kwa kuwa tangu mwaka 2011 nafasi ya
majadiliano ilikuwepo.MAGUFULI
Akasisitiza kwa kusema “Tangu mwaka 2011 walipaswa kujiandaa
kama miaka yote hiyo wameshindwa kufanya majadiliano hii miezi mitatu
wanayoiomba ndio wataweza? Acha bunge lifanye kazi yake kwa kuwa tayari
muswaada huo umekwisha wasilishwa na naomba nikuhakikishie sitakuwa mnafiki
wakileta mezani kwangu nitasaini mara moja”.
Post a Comment