SANCHEZ AINGIA MATATANI UKWEPAJI WA KODI
Na: Imani Kelvin Mbaga
Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anaechezea klabu ya Arsenal ya nchini England Alexis Sanchez, anatuhumiwa kwa jaribio la kukwepa kodi akiwa mchezaji wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2014.
Kwa mujibu wa gazeti linalotolewa katika jiji la Barcelona lijulikanalo kama El Periodico, Sanchez anatuhumiwa kufanya jaribio la kukwepa kodi hadi kufikia kiasi cha Euro 983,443 sawa na kiasi cha paundi 888, 736 kwa miaka hiyo mitatu.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Sanchez anaweza akahukumiwa kifungo jela endapo atakutwa na hatia ya ukwepaji huo wa kodi kwa mujibu wa sheria za Hispania.
Sanchez mwenye umri wa miaka 27 anatuhumiwa kuhamishia haki za hadhi yake kwa kampuni ya siri iliyoko katika visiwa vya Malta ikijulikana kwa jina la Numidia Trading.
Hiyo siyo mara ya kwanza kwa wachezaji wa Barcelona kutuhumiwa kwa kosa la ukwepaji wa kodi katika kipindi cha miaka ya karibuni ambapo Javier Mascherano na Lionel Messi walikutwa na kadhia hiyo ya kushtakiwa kwa ukwepaji wa kodi ambapo Messi alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 na kupiogwa faini ya kiasi cha Euro milioni 1.7 mwezi mei mwaka huu.
Huenda Sanchez akakutana na adhabu kama hiyo endapo atapatikana na hatia katika kesi inayomkabili na hadi sasa uchunguzijuu ya tukio hilo unaendelea
Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anaechezea klabu ya Arsenal ya nchini England Alexis Sanchez, anatuhumiwa kwa jaribio la kukwepa kodi akiwa mchezaji wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2014.
![]() |
mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez |

Post a Comment