YANGA YAFIA SOKOINE,SIMBA YAPAA KAMBARAGE
Na: Imani Kelvin Mbaga
Ligi kuu ya kandanda Tanzania bara "VPL" leo iliendelea katika jumla ya viwanja sita huku viwanja viwili ndiko ambako macho na masikio ya mashabiki wengi yalielekezwa kutokana na kuhusisha mafahali wa soka la Tanzania Simba na Yanga ambao wanafukuzana kileleni mwa msimamo wa ligi kwa sasa.
Yanga walisafiri kwenda Mbeya kuwavaa Mbeya City wakati mahasimu wao katika soka la Tanzania walisafiri mkoani Shinyanga kukwaana na na Stand United maarufu kama chama la wana au kiboko ya vigogo kwa msimu huu.
Katika dimba la uwanja wa sokoine Yanga wamepoteza mechi ya pili toka ligi ianze baada ya kunyamazishwa na wenyeji wao Mbeya City walioonekana kuimarika mno katika mechi ya leo hasa kila mara walipopanga mashambulizi yao langoni mwa Yanga.
Mashujaa wa leo kwa upande wa Mbeya City walikuwa ni Kenny Ally na Hassan Mwasapili ambao walifunga magoli ya MCC katika dakika ya 6 na 35 kabla ya Donald Ngoma hajafunga goli la kufutia machozi kwa upande wa Yanga katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.
Yanga walioneka kucheza vibaya katika kipindi cha kwanza ukilinganisha na kipindi cha pili ambapo Mbeya walikuwa vizuri katika kipindi cha kwanza kuliko cha pili licha yya kuonyesha nidhamu kubwa ya ukabaji
Kule Shinyanga katika uwanja wa Kambarage Simba wameongeza pengo la pointi 8 dhidi ya Yanga kwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ngumu ya Stand United,goli la Shiza Kichuya kwa njia ya mkwaju wa pelnat baada ya Laudt Mavugo kuangushwa ndani ya eneo la hatari la Stand United
Hilo lilikuwa ni goli la tisa kwa Shiza Kichuya katika msimu wake wa kwanza akiichezea Simba.
Matokeo mengine ni
Ruvu Shooting !-0 African Lyon
Toto 0-1 Azam
Ndanda 1-0 Prisons
Ligi kuu ya kandanda Tanzania bara "VPL" leo iliendelea katika jumla ya viwanja sita huku viwanja viwili ndiko ambako macho na masikio ya mashabiki wengi yalielekezwa kutokana na kuhusisha mafahali wa soka la Tanzania Simba na Yanga ambao wanafukuzana kileleni mwa msimamo wa ligi kwa sasa.
![]() |
Shiza Kichuya |

Post a Comment