SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI ABUBAKARI ZUBERI APOKEA TAARIFA YA TUME ALIYOIUNDA KUFATILIA MALI ZA BAKWATA NCHINI
By Jumanne S. Juma
Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Zuberi Bin Ally leo amekabidhiwa ripoti na tume aliyoiunda miezi mitatu iliyopita, kufuatia tamko la rais wa jamuhuri ya muungano Dk. John Pombe Magufuli kutamka kuwa anataka kusaidia kuzirudisha mali zilizopolwa katika taasisi za dini hapa nchini.

Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Zuberi Bin Ally
Kamati hiyo ya watu sita ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sheikh
Abubakari Kharid, Makamo mwenyekiti Sheikh Issa Othman Issa, Sheikh katibu
Salim Abeid na wajumbe watatu Herera Tabu Kawambwa, Omary Ige, na Khamisi
Mataka, imefatilia taarifa za mali za waislamu kwa mkoa wa dare s salaam pekee
kwa kipindi cha miezi mitatu na kukabidhi ripoti hiyo.
Awali kabla ya kukabidhi ripoti hiyo makamu mwenyekiti Issa Othman
Issa alisema kuwa tume hiyo imefatilia mikataba na mali za baraza la waislamu
na kwa sasa wamekamilisha ripoti ya mkoa wa Dar es salaam.
Akikabidhi ripoti hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa tume hiyo Makamo
mwenyekiti Issa Othman Issa ametoa ombi
kwa mufti la kuongezewa miezi mingine mitatu ili kuweza kukamilisha kazi hiyo
kwa nchi nzima.
Akipokea ripoti hiyo Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi,
amekubali kuiongezea muda tume hiyo, na ameongeza kuwa ataanza kuipitia ripoti
hiyo, kuanzia kesho na mara baada ya kukamilisha kuipitia ripoti hiyo atatoa
tamko kwa watanzania juu ya ripoti hiyo.
Post a Comment