STEPS WAJA NA AFRO BOX KUPELEKA FILAMU KWA WATEJA WAO
Myovela Mfwaisha, meneja matukio wa kampuni ya Steps Entertainment |
Na; Imani Kelvin Mbaga
Kampuni
inayojihusisha na usambazaji na filamu nchini,ijulikanayo kama Steps
Entertainment, imetangaza kuingiza sokoni kwa namna ya tofauti na kisasa
zaidi filamu mpya iitwayo “SIRI YA MOYO” inayotarajiwa
kuzinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Salum Saleh, mtayarishaji wa filamu ya SIRI YA MOYO |
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo, meneja wa
matukio wa kampuni hiyo, Myovela Mfwaisha, alisema kuwa kampuni yake imeamua
kuipa thamani zaidi sekta ya filamu na kuisogeza kwa wadau kwa njia ya kisasa
na rahisi zaidi kuifikia.
“Tunachotaka
kufanya ni kuhakikisha kuwa kila mtu anapata kwa urahisi kuona filamu zetu na
kuondoa vikwazo na vizuizi vinavyowakabili watu katika kufurahia kazi zetu”
Alisema Myovela.
Man D mmoja kati ya watu waliocheza filamu ya SIRI YA MOYO |
Akizungumzia
njia itakayotumika, Myovela alisema kuwa wametengeza njia rahisi ya kuzifikisha
filamu kwa kutumia simu za kiganjani, ambapo mtumianji wa simu za kufuta “smart
phone” atatakiwa kuwa na program ya Afro
box ambayo ni lazima aipakue kwenye simu yake kuweza kuangalia filamu
mbalimbali kwa urahisi.
Akifanunua
zaidi meneja huyo alisema pia kuwa filamu hiyo ya SIRI
YA MOYO itaanza kuonyehwa kwenye ukumbi wa sinema kabla ya kuanza
kupatikana katika program hiyo ya simu na kusambazwa maeneo mbalimbali kwa
wateja na wapenzi wa filamu nchini.
kutoka kulia ni Man D, Salum Saleh na Myovela Mfwaisha |
Naye
mtayarishaji wa filamu hiyo, Salumu Saleh, alisema wameitengeneza filamu hiyo
ili kukidhi mahitaji na vigezo vya viwango vya kimataifa, na kwamba kupata
nafasi ya kuonyesha filamu hiyo kwenye ukumbi wa sinema ni uthibitishio wa
ubora wa kazi yake na kwamba huo ni mwanzo wa kuipeleka mbele tasnia hiyo.
Post a Comment