Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

ARSENAL USO KWA USO NA BAYERN ULAYA, MAN UNITED YATUPWA UFARANSA




na Imani Kelvin Mbaga



Timu ya Arsenal ya England imejikuta ikiingia mdomoni mwa timu ya Bayern Munich ya Ujerumani katika hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kufuatia droo iliyochezeshwa leo katika mji wa Nyon

Arsenal maarufu kama washika bunduki wa jiji la London wamejikuta wakifadhaishwa na droo hiyo kutokana na juhudi kubwa waliyoifanya kumaliza wa kwanza katika hatua ya makundi ili kuepuka kukutana na timu ngumu lakini juhudi hizo zimeishia kukutana na Bayern Munich ambao wameshika nafasi ya pili.

Arsenal na Bayern wamekutana mara sita katika miaka minne ambapo Bayern wamefunga jumla ya magoli 10 huku Arsenal wakifunga jumla ya magoli 7 katika mechi zote walizokutana kama inavyoonekana hapa chini.
2012-13 (16 BORA)
Arsenal 1-3 Bayern Munich
Bayern Munich 0-2 Arsenal
2013-14 (16 BORA)
Arsenal 0-2 Bayern Munich
Bayern Munich 1-1 Arsenal
2015-16 (MAKUNDI) 
Arsenal 2-0 Bayern Munich
Bayern Munich 5-1 Arsenal  
Droo ya kupanga nani acheze na nani katika hatua ya mtoano huziweka timu zilizoongoza makundi yao katika sehemu moja na zile zilizoshika nafasi ya pili katika hatua ya makundi huwekwa pamoja ili kuepuka kuzikutanisha timu zilizoshika nafasi sawa katika makundi yao.

Wakati huo huo timu za Hispania zimeendelea kutawala soka la Ulaya baada ya kutajwa zaidi katika droo ya upangaji wa mechi za mtoano za vilabu barani humo, zinazohusisha michuano ya klabu bingwa na kombe la Uropa, ambapo nchi hiyo imeingiza timu 7 kati ya timu 48 kutoka mataifa yote.

Timu za Hispania zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano kutoka nchi hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi wa kombe la klabu Bingwa barani humo, Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid na Sevilla katika ligi ya mabingwa, kwa upande wa Uropa ni Athletic Bilbao, Celta de Vigo na Villa Really.

England imefanikiwa kuingiza timu tano katika hatua hiyo, baada ya Arsenal, Leicester City na Manchester City kusonga mbele katika klabu bingwa, wakati ambapo Manchester United na Tottenham Hotspurs zikisonga katika michuano ya Uropa.
Hatua ya mtoano ya michuano ya vilabu barani Ulaya inatarajiwa kuanza kuchezwa tar 14 na 15 mwezi Februari ambapo timu zote zilizo shika nafasi ya kwanza katika makundi yao zitaanzia ugenini na kumalizia nyumbani kama inavyoonekana katika ratiba kamili hapa chini
anchester City vs Monaco 
February 21 - Manchester
March 15 - Monaco
Real Madrid vs Napoli
February 15- Madrid
March 7 - Naples
Benfica vs Borussia Dortmund
February 14 - Lisbon
March 8 - Dortmund
Bayern Munich vs Arsenal 
February 15 - Munich
March 7 - London 










 Porto vs Juventus
February 22 - Porto
March 14 - Turin
Bayer Leverkusen vs Atletico Madrid
February 21 - Leverkusen 
March 15 - Madrid 
Paris Saint Germain vs Barcelona
February 14 - Paris
March 8 - Barcelona 
Sevilla vs Leicester City 
February 22 - Seville
March 14 - Leicester 

RATIBA YA MICHUANO YA MTOANO UROPA

RSC Anderlecht V Zenit St Petersburg
0










Astra Giurgiu V KRC Genk
18:00





Athletic Bilbao V Apoel Nicosia
18:00





AZ Alkmaar V Lyon
18:00





Borussia Mönchengladbach V Fiorentina
18:00





Celta Vigo V Shaktar Donetsk
18:00





FC Rostov V Sparta Prague
18:00





FK Krasnodar V Fenerbahçe
18:00





Hapoel Be'er Sheva V Besiktas
18:00





KAA Gent V Tottenham Hotspur
18:00




Legia Warsaw V Ajax 18:00











Ludogorets Razgrad V FC Copenhagen
18:00





Manchester United V Saint-Étienne
18:00





Olympiakos V Osmanlispor
18:00





PAOK Salonika V FC Schalke 04
18:00






Villarreal V Roma
18:00


No comments

Powered by Blogger.