Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

ARSENAL WATINGA 16 BORA KWA STAILI HUKU PEREZ AKITUMA SALAMU KWA WENGER



 
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia ushindi dhidi ya FC basel
Na: Imani Kelvin Mbaga

Washika bunduki wa jiji la London, timu ya Arsenal jana walifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa staili ya aina yake baada ya kufanya kile walichoshindwa kufanya kwa miaka takribani mine iliyopita baada ya ya kufanikiwa kuongoza kundi.
Jana zilichezwa mechi za mwisho katika hatua ya makundi, ambapo makundi A, B, C  na D yalimaliza michezo yao na kushuhudia timu nane kutoka makundi hayo zikikata tiketi kucheza hatua ya 16 bora wakati timu nne zikirudi kucheza EUROPA na timu nne kutupwa nje ya mashindano hayo msimu huu.
Arsenal  walifanikiwa kupata nafasi ya kuongoza kundi A kwa kujikusanyia  alama 14 mbele ya PSG ya Ufaransa iliyomaliza na alama 12 katika kundi hilo. Arsenal walimaluizia mchezo wao wa mwisho kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Fc Basel ya Uswizi huku PSG wakiambulia sare ya 2-2 nyumbani dhidi ya Ludogorates.
Tangu mwaka 2005 Arsenal hawajawahi kumaliza hatua ya makundi bila kupoteza mchezo kama ilivyotokea safari hii, na miaka mine iliyopita mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakililia angalau kuiona timu yao ikimaliza ya kwanza katika hatua ya makundi ili kuepuka kukumbana na vigogo katika hatuia ya mtoano.
Naye mchezaji aliyesajiliwa msimu huu kutoka Deportivo La Coruna, Lucaz Perez, alijiwekea rekodi mpya baada ya kufunga mabao matatu yaani “hat trick” kailka mchezo huo, na kuwa mchezaji wa sita wa Arsenal kufunga “hat trick” katika michuano hiyo baada ya Thiery Henry, Niklas Bendtiner, Olivier Giroud, dan Wellbeck, Mesuit Ozil nayeye Lucaz Perez.
Timu zilizofanikiwa kusonga mbele baada ya mechi za jana za makundi hayo ni kundi A, Arsenal na Psg, kundi B, Napoli na Benfica, kundi C, Barcelona na Manchester City, kundi D, Atletico Madrid na Bayern Munich.
Leo timu nyingine nane zinatarajiwa kujulikana baada ya michezo ya makundi E,  F, G na H kuchezwa kasha UEFA watafanya droo kujua nani atakutana na nani katika hatua hiyo ya 16 bora mwanzoni mwa mwaka ujao.
Mlinda mlango wa Arsenal David Ospina akiokoa hatari langoni mwake katika wa mchezo wa jana dhidi ya fc Basel
 
Mshambuliaji wa Arsenal, Lucas Perez akishangilia moja ya mabao aliyofunga jana katika mchezo dhidi ya Fc Basel

No comments

Powered by Blogger.