Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

TPA:TUMEDHAMIRIA KUIBORESHA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) katika kuhakikisha huduma zinazotolewa na bandari ya Dar es Salaam zinaboreshwa, imeanza ukarabati utakaowezesha kushusha mizigo Tani milioni 26 ifikapo 2025 kutoka tani 15 zinazoshishwa sasa.

Jumla ya Sh. bilioni 132 zimetolewa kama msaada na Taasisi ya Trade Mark iliyofadhiliwa na nchi ya Marekani kwa ajili ya ukarabati wa bandari hiyo hadi ifikapo 2019 itakapokamilika.
Mkurugenzi wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, aliyaeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini makubalino ya ukarabati wa bandari hiyo na Taasisi ya Trade Mark.

Alisema pia ifikapo 2030 wanatarajia kuwa, bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kushusha mizigo Tani milioni 40 hadi 45 kutokana na kupanuka kwake na kuwezesha meli kubwa kuingia nchini.
“Tumejipanga kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano kwa kuwa kila kitu kimeanza na kila kitu kitakamilika. Kazi imeshaanza na yule ambaye ameshapita bandarini ameona mabadiliko ya mageti na camera za systetv angalia na barabara za ndani kimsingi kazi hii ilianza baada ya makubaliano na matarajio kazi yetu itakamilika kabla ya 2019,” alisema.
Kakoko alisema kazi hiyo itaenda sambamba na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kusaidia kazi bandari ya Dar es Salaam pindi itakapoongeza idadi ya mizigo ifikapo 2025.
Alisema mizigo inayoingia kwenye bandari ya Dar es Salaam ni asilimia 90 hadi 95 ya mizingo yote na kwamba ukarabati utakaofanyika ni kuboresha miundombinu na kuweka mfumo wa Tehama.
Kakoko alisema eneo la Lambo lina kina kidogo na dethi ina urefu wa moja hadi saba na kina kidogo cha mita sita hadi saba na kwamba wanachofanya ni kuboresha, kuongeza kina kirefu ili meli kubwa zenye uzito mkubwa kutia nanga nchini.

Naye Mkurugenzi wa Trade Mark, nchini, John Ulanga, alisema lengo la kuwezesha kuboresha bandari hiyo ni kuchangia kukua kwa uchumi wa Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.