IBARAHIMOVIC: SIKUPIGA MTU TEKE LA KICHWA
![]() | ||
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic akiwa amemwangukiwa mlinzi wa kushoto wa timu ya Everton seamus Coleman wakti wa mechi kati ya timu hizo iliyoisha kwa sare ya goli 1-1. |
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amekanusha vikali kwamba alimpiga teke la kichwani kwa makusudi mlinzi wa kushoto wa klabu ya Everton, Seamus Coleman kitendo kilicjiosababisha maumivu yaliyomtoa nje ya mchezo huo Coleman.
Akizungumza na kituo cha runinga cha klabu yake, Ibrahimovic alisisitiza kuwa tukio hilo lilikuwa tukio la bahati mbaya na kwamba hakukusudia kumuumiza mchezaji huyo na kwamba hilo ni jambo linaloweza kutokea katika mchezo wa mpira wa miguu.
"Nilimsikia mchambuzi mmoja akisema, nimempiga mtu teke la kichwani, hii si kweli kwani yeye alijaribu kunivuta chini nami nilijaribu kumkwepa ili nisimjeruhi, kwani najua jinsi ya kumpiga mtu kichwani na hii ilimkuwa ni bahati mbaya tu" Alisema Ibrahimovic
Mshambuliaji huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa Taekwondo, aliruka juu kugombea mpira mna mlinzi huyo wakati wa kipindi cha pili cjha mchezo baina ya timu hizo katika dimba la uwanja wa Gudson Park na mechi hiyo kwisha kwa goli 1-1 goli lililofungwa naye Ibrahimovic.
Akizungumzia matokeo ya mchezo huo,Ibrahimovic alisema kuwa siyo matokeo mabaya kwakuwa hawakupoteza mchezo na kwamba wataendelea kupambana hadi pale watakapopata kile wanachokitaka katika ligi hiyo ikiwa ni pamoja na ubingwa na nafasi ya kucheza kalbu bingwa barani humo
Post a Comment