NDANDA YATUMIKA KAMA NGAZI KUIPELEKA YANGA JUU
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara, Yanga Sc wamefanikiwa kunyakua point tatu muhimu katika mbio za kuutetea ubingwa wao katika msimu huu wa 2016/17, baada ya kuwanyuka "wamakonde" wa Ndanda kutoka mkoani Mtwara kwa ushindi wa magoli 4-0 kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo.
Mchezo huu ulionekana kabla kuwa ungekuwa mgumu kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana, lakini pia matokeo ya hivi karibuni kwa timu zote yalionekana kubashiri ugumu wa mchezo huo wa leo.
Yanga iliingia uwanja baada ya kubanwa mbavu katika mchezo uliopita na African Lyon na kulazimishwa sare ya 1-1 kitendo kilichowapa nafasi mahasimu wao Simba Sc kutanua wigo wa point hadi kufikia pointi nne kileleni, kitendo kilichosababisha baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kongwe kuwazonga wachezaji wa timu hiyo kwa madai ya hujuma.
katika mchezo wa leo Yanga waliianza karamu ya magoli dakika ya 4 tu ya mchezo baada ya mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma kuunganishwa kwa kichwa mpora wa kona uliopigwa na Simon Msuva, hadi kufikia dakika ya 26, Yanga walikua mbele kwa mabao 3-0 kwa magoli ya Donald Ngoma aliyefunga mara mbili na amiss Tambwe.
Dakika za mwisho za mchezo huo mlinzi wa Yanga Vincent Bossou aliiandikia Yanga goli la 4 kwa kichwa na kuhitimisha karamu hiyo ya magoli ambapo sasa Yanga wamefikisha jumla ya pointi 40 ikiwa ni pointi moja tu nyuma ya Simba ambao wapo kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi 41 lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi utakaochezwa kesho katika dimba la uwanja wa Uhuru .
Mechi kati ya Yanga na Ndanda imekuwa ni mechi yenye upinzani katika siku za karibuni hususani toka Ndanda ilipopanda ligi kuu imekuwa ikionekana kutoa upinzani mkali kwa Yanga tofauti na ilivyoonekana katika mchezo wa leo ambapo timu hiyo ilizidiwa katika kila idara .
![]() |
| Deus Kaseke akiruka juu kupiga mpira kwa kichwa wakti wa mpambano kati ya Yanga na Ndanda |

Post a Comment